SERIKALI ya Rais John Magufuli imewafuta machozi wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe kwa kuwapa gari kwa ajili ya usafi. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).
Alhaji Aboud Jumbe ameacha wake wawili ambao wamekabidhiwa gari hiyo na George Mkuchika leo hii jijini Dar es Salaam ambapo ni utekelezaji wa Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Viongozi wa Kisiasa Na. 3 ya mwaka 1999 na Marekebisho yake ya mwaka 2005 inayoelekeza utoaji wa stahili kwa wajane wa viongozi wa Kitaifa Wastaafu.
Sambamba na kuenzi mchango Aboud Jumbe, Mkuchika amesema kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, stahili za wajane kwa viongozi wa Kitaifa Wastaafu ni pamoja na malipo ya pensheni, malipo ya posho ya matunzo ya kila mwezi, gharama za matibabu katika hospitali zilizomo nchini na kupatiwa huduma ya usafiri.
Mkuchika amesema, alikuwa ni kiongozi mahiri, jasiri na mchapakazi aliyeweza kutuliza machafuko yaliyowahi kutokea Zanzibar na amefanya kazi ya kuwaunganisha watanzania.
Ziara Mkuchika ni mwendelezo wa kuwajulia hali viongozi wa Kitaifa Wastaafu kwa lengo la kuboresha huduma wanazopatiwa na Serikali.
Leave a comment