Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali: Watumishi wa Acacia wapo salama
Habari za SiasaTangulizi

Serikali: Watumishi wa Acacia wapo salama

Kampuni ya Acacia
Spread the love

SERIKALI imekanusha madai ya Kampuni ya Madini ya Acacia, ya kwamba usalama wa watumishi wake uko hatarini kutokana na kuwindwa na vyombo vya dola, kwa lengo la kushtakiwa mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Acacia kupitia taarifa iliyochapisha kwenye tovuti yake, inadai kuwa, Serikali imeshinikiza watumishi wake wawili katika Migodi ya North Mara, Bulyanhulu na Pangea (Buzwagi), Deo Mwanyika na Alex Lugendo kufikishwa mahakamani na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tarehe 17 Oktoba 2018 kwa makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Kufuatia kushtakiwa kwa watumishi wake, Acacia kupitia taarifa yake hiyo, inaeleza kuwa imefungua shauri katika Baraza la Usuluhishi ili kulinda maslahi ya wadau wa kampuni zake.

Taarifa iliyotolewa jana tarehe 25 Oktoba 2018 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Biswalo Mganga ilitoa ufafanuzi wa madai hayo, ikisema kuwa, kufikishwa mahakamani kwa watumishi hao hakutokani na shinikizo lolote la serikali, bali ofisi yake inafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya sheria.

Mganga kupitia taarifa hiyo alifafanua kuwa, kuhusika au kutohusika kwa watumishi na kampuni tajwa kwenye kesi hizo kutaamuliwa na mahakama ambayo ndiyo chombo cha utoaji haki kwa mujibu wa katiba na sheria. Na kwamba mikataba ya kulinda uwekezaji iliyoingiwa kati ya Serikali ya Tanzania na nchi yoyote haizuii na siyo kinga ya kutofunguliwa kesi ya jinai kwa kampuni, mwekezaji au mtumishi wa mwekezaji.

“Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefungua kesi hizo kutokana na kuridhishwa na ushahidi uliopatikana unaoonesha matendo ya kijinai ya watumishi hao, kwa nafasi zao ndani ya makampuni hayo kwa nyakati zilizotajwa kwenye hati ya mashtaka na ushiriki wa makampuni hayo wakati huo ambapo uchunguzi umebaini kuwa walivunja sheria,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa, watumishi hao siyo wa kwanza kushtakiwa mahakamani, na kwamba walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

“Kesi hizi hazina mahusiano na shauri/mashauri yaliyofunguliwa katika Baraza la Usuluhishi na makampuni ya Bulyanhulu na Buzwagi. Na vile vile uwepo wa mashauri kwenye mabaraza ya usuluhishi hakuzuii Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa mujibu wa Katiba na Sheria kufungua shauri la jinai kwa mtu au kampuni,” iliendelea kufafanua taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!