January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali wasilikiza mapendekezo ya walemavu

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeendelea kusikiliza changamoto na mapendekezo ya makundi mbalimbali ya walemavu kwa lengo la kutekeleza mahitaji maalum kwa kila kundi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Mapendekezo hayo yamepokelewa leo na Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Possi katika ofisi zake wakati wa mkutano maalum wa kusikiliza changamoto za walemavu.

Akizungumza na wanahabari Dk. Possi amesema kuwa ili kutekeleza masuala mbalimbali muhimu ya walemavu ni vyema serikali ikawa na mipango maalum inayowezesha kutambua mahitaji yao.

Amesema kuwa makundi ya walemavu yapo katika nyanja tofauti na kila kundi linamahitaji yake hivyo sheria namba 9 ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 inayotaka ushirikishwaji wa walemavu katika maamuzi itasaidia kupata ufumbuzi wa matatizo kwa kila kundi la walemavu kwa njia ya kuwashirikisha kutoa maamuzi na maono.

“Sio kila mlemavu anahitaji wheelchair, ili kupata uhakika wa mipango wanayotaka kufanya ni lazima serikali kuwa angalifu kujua mahitaji muhimu ya kila aina ya ulemavu,” amesema Dk. Possi.

Naye Mwenyekiti wa Shirika la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Amon Anastaz amezitaka wizara zote serikalini kukumbuka makundi ya walemavu wakati wa kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza ushirikishwaji wa makundi maalum ya walemavu.

Anastaz ambae ndiye Mwenyekiti wa kikosi kazi kilichoandaa mapendekezo kwenda kwa naibu waziri, amesema kuwa kutokuwepo kwa takwimu maalum ya idadi ya walemavu nchini ndio changamoto kubwa inayopelekea serikali kushindwa kumaliza changamoto kwa watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa ajira ni changamoto kubwa kwa upande wa walemavu hivyo mapendekezo hayo yameomba serikali kusimamia maslahi ya walemavu katika ajira.

error: Content is protected !!