August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Utalii umechangia 17%

Spread the love

SERIKALI imesema kwamba, Sekta ya Maliasili na Utalii imechangia kiasi cha asilimia 17 katika pato la Taifa, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Ramo Makani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Agustino Masele, Mbunge wa Mbogwe (CCM).

Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua kuwa, serikali ina mpango gani wa kuboresha miundo mbinu ya sekta ya utalii ikiwemo barabara na hoteli.

Makani amesema kuwa, mchango wa sekta hiyo ya utalii katika uchumi na maendeleo ya Taifa ni mkubwa hususani katika kuipatia serikali fedha nyingi.

Amesema, wizara inaamini kwamba kwa kuboresha miundombinu , vivutio na utoaji huduma, sekta hiyo inaweza kuchangia zaidi katika pato la Taifa na upatikanaji wa fedha za kigeni .

Amesema, kwa mujibu wa ibara ya 33(c) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020 inasisitiza juu ya umuhimu na inaelekeza serikali kuboresha miundombinu ndani ya mapori ya hifadhi ya akiba.

Amesema, miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha kuwa, mazao yatokanayo na maliasili yanaendelea kuchangia katika pato la Taifa.

Naibu huyo amesema, mpango wa serikali kuhusu uboreshaji wa miundombinu katika pori la akiba la Kigosi/ Muyoyosi ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa Mamlaka ya wanyama pori wa mwaka 2016/17.

 

error: Content is protected !!