July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Ruksa kutumia wakalimani

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose - Migiro

Spread the love

SERIKALI imesema watuhumiwa wote wenye kesi kubwa ambazo zinasikilizwa Mahakama Kuu, wana uhuru wa kuwatumia wakarimani pale ambapo wanashindwa kuelewa lugha ya Kiingereza. Aanandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose – Migiro, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) leo.

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia Watanzania ambao wanakabiliwa na kesi katika mahakama kuu ambao hawawezi kusoma wala kujua lugha ya Kiingereza kuwawapatia wakarimani.

“Wapo baadhi ya Watanzania ambao wanakabiliwa na kesi katika mahakama kuu na kesi hizo uendeshwa kwa lugha ya Kiingereza na kwa kuwa wapo baadhi ya Watanzania ambao hawajui lugha hiyo, je serikali ina mpango gani wa kuwawekea wakarimani ili wajue kinachoendelea katika kesi hizo,”amehoji.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Rosweeter Kasikila (CCM), alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa mikataba ya Itifaki na maazimio ya kimataifa na kikanda inatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Akijibu maswali hayo, Dk. Migiro amesema Watanzania wanaokabiliwa na kesi mbalimbali ambazo zinasikilizwa kwa lugha ya Kiingereza wana uhuru wa kutumia wakarimani.

Mbali na hilo, amesema ni dhamira ya serikali kuhakikisha inatafsiri mikataba, Itifaki na maazimio mbalimbali katika lugha ya Kiswahili.

Kutokana na umuhimu wake, Dk.Migiro ametoa rai kwa Wizara, Idara na Taasisis za serikali zinazotekeleza moja kwa moja mikataba na Itifaki mbalimbali au kikanda kuitafsiri katika lugha ya Kiswahili ili kuwezesha wananchi wengi kuielewa na kuifanyia rejea.

error: Content is protected !!