June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali okoeni wakulima Dodoma

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuwawezesha wakulima mkoani Dodoma, ili waweze kulima kilimo cha kisasa badala ya kulima kilimo cha mazoea na kisichokuwa na tija, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa na Sebastian Msola, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kibaigwa flower supplies Ltd, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya kuishauri serikali kuwawezesha wakulima kulima kilimo bara sambamba na unenenepeshaji wa mifugo.

Msola amesema kuwa, kwa hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi ilivyo, haiwezekani wakulima wakaendelea kutegemea kilimo cha mvua na badala yake wakulima wanatakiwa kulima kwa teknologia mpya ambayo ni ya umwagiliaji.

“Kilimo lazima kiwe cha kibiashara, badala ya kuwa kilimo cha kijikimu. Lazima yawepo mazao yenye ubora ambayo yanatokana na kilimo cha kisasa.

Nchi ya viwanda inatengenezwa na uzalishaji bora wa mazao ambayo yanapatikana nchini badala ya kuagiza mazao kutoka nje ya nchi, jambo linalosababisha bidhaa za ndani kukosa soko,” amesema Msola.

Amesisitiza kuwa ni lazima wakulima walime kilimo chenye ufanisi mkubwa ambacho mazao yake yataweza kuingia katika ushindani wa soko la dunia.

“Kutokana na hali  ya ukame wa mara kwa mara kwa mikoa ya Kanda ya Kati, wakulima wa mikoa hiyo wanashauriwa kuacha kulima mazao yasiyostahimili ukame na badala yake kulima zao la kibiashara la aina ya Katam (Alizeti yenye miiba), inayoendana na hali ya hewa,” amesema.

error: Content is protected !!