Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Namaingo ni neema, itumieni vizuri  
Habari Mchanganyiko

Serikali: Namaingo ni neema, itumieni vizuri  

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti (DC), Gulamhussein Shabani Kifu akipanda mti
Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Kibiti (DC), Gulamhussein Shabani Kifu amewataka wananchi wa Kijiji cha Ruaruke wilayani Kibiti pia wananci wote kwa ujumla kuitumia vizuri Namaingo katika kujiletea maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kibiti … (endelea).

Akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ruaruke katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Jumanne 12 Machi 2019 katika shamba la Namaingo, lililopo kitongoji cha Mbawa, DC Kifu amesema, Namaingo kuamua kuwekeza miradi yao wilayani Kibiti ni neema kubwa kwa wilaya yake na wananchi wanapaswa kuitumia vema neema hiyo.

Kampuni ya Namaingo Business Agency chini ya mkurugenzi wake, Biubwa Ibrahim, inatoa elimu kwa wanachama wake kujiunga pamoja na kufanya miradi ya uzalishaji, hasa katika nyanja za kilimo, ufugaji na kuongeza thamani mazao wanayozalisha. Pia inawaunganisha wanachama na wataalamu wa kilimo na ufugaji, inawatafutia masoko pamoja na ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

“Nawashauri mumtumie vizuri Biubwa na wasaidizi wake, mkitaka ufugaji wa kuku atawapa elimu, ufugaji wa nyuki atawapa elimu na ukija mradi hakikisheni mnaufanya vizuri.” Amesisitiza DC Kifu.

Wanachama wa Namaingo wameanza uwekezaji wa miradi miwili katika wilaya ya Kibiti. Ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Kikale, walikoanza na mizinga 200 lakini lengo likiwa kuwekeza mizinga 5,000 na ukulima wa zao la korosho katika kijiji cha Ruaruke A, tayari wamesafisha ekari zaidi 80, ambazo upandaji wake wa mikorosho umezinduliwa juzi Jumanne na DC wa Kibiti.

Wakati anawahutubia wananchi, DC Kifu amesema Biubwa ametueleza anapenda kuona watu wanabadili mitazamo yao ili waende kwenye utajiri, ni vigumu matajiri kuona wanaendesha semina na mafunzo kama haya ya kuwafanya watu wasiwe masikini kama anavyofanya Biubwa, matajiri wao wanazalisha bidhaa wanatuletea tununue.

“… kwanini matajiri wasituite kwenye vikao kama hivi kutubadili mitazamo yetu ya ufikiri na sisi tuweze kupata mali? Lakini Biubwa anayetuita na kutupa elimu tunampiga vita na matusi mengi, mara ooh wewe mwanamke, hivi ndugu zangu hakuna wanawake wema na wachamungu?” Anauliza DC kwa msisitizo.

DC amewaonya wafugaji kuacha mara moja kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima na kumuagiza mtendaji wa kijiji kuhakikisha anakuwa na orodha ya wafugaji wote na aina ya mifugo wanayofuga. Amesema hakuna mfugaji yeyote atakayeingiza mifugo kwenye shamba la mtu akaachwa.

Pia akawapa onyo wavuna miti na wachoma mkaa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na vibali walivyopewa, hakuna mvuna miti wala mchoma mkaa anayeruhusiwa kufanya shughuli hizo maeneo yenye miradi ya kilimo au ufugaji wa nyuki, atakayejaribu kufanya hivyo serikali haitamuacha.

Ziara ya mkuu wa wilaya ya Kibiti katika kijiji cha Ruaruke yaliko mashamba ya Namaingo iliambatana na viongozi kadhaa wa wilaya ya hiyo akiwemo Katibu Tawala, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na makamu wake, Mbunge wa jimbo la Kibiti Ally Ungando, meneja wa TFS wilaya ya Kibiti, baadhi ya madiwani na watendaji wa vijiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!