December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Mwaka 2015 – 19 tumeajiri watu 184,141

Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira.

Spread the love

SERIKALI imesema, imeajiri watu 184141, kuanzia mwaka 2015 hadi 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Takwimu hizo zimetolewa leo tarehe 5 Novemba 2019, bungeni jijini Dodoma na Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira.

Wakati huo huo, Mavunde amesema miradi ya maendeleo imetoa ajira  787405, na sekta binafsi imeajiri watu 646,466.

“Kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 serikali kupitia taasisi zake imeajiri 184,141, ajira zilizotolewa kupitia miradi ya maendeleo ya serikali ni 787405, na ajira  646,466 zilitolewa na sekta binafsi,” amesema Mavunde.

Mavunde ametoa takwimu hizo wakati akijibu swali la Anna Gidarya, Mbunge Viti Maalumu mkoani Manyara.

Mavunde ametoa takwimu hizo wakati akijibu swali la Anna Gidarya, Mbunge Viti Maalumu mkoani Manyara, aliyehoji mkakati wa serikali katika kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu.

Gidarya amesema, kuna kundi kubwa la vijana halina ajira kwa zaidi ya miaka mitatu, na kudai kwamba serikali imekuwa kimya katika kutoa majibu kuhusu changamoto hiyo.

Lakini, swali hilo limejibiwa na Mavunde, aliyesema kwamba serikali inaendelea kuajiri watu kupitia taasisi zake kila mwaka, kwa kuzingatia mahitaji na bajeti. Pia, miradi ya maendeleo pamoja na ongezeko la shughuli za kiuchumi, imeongeza wigo wa utoaji ajira.

error: Content is protected !!