Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Mradi wa REA haulipi fidia
Habari Mchanganyiko

Serikali: Mradi wa REA haulipi fidia

Spread the love

SERIKALI imesema, hakuna malipo ya fidia kwenye maeneo ya wananchi,yanayopitiwa na mradi wa usambazaji umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Anaripoti Regina Mkonde …(endeea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 10 Juni 2019 bungeni jijini Dodoma na Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Nishati wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum mkoani Arusha, Catherine Magige.

Swali la Magige lilihoji kwamba, lini serikali itakamilisha mchakato wa ulipaji fidia kwa wananchi zaidi ya 2,000 wa Wilaya ya Longido na Monduli mkoani Arusha, ambao maeneo yao yalipitiwa na mradi wa REA.

Akijibu swali hili, Mgalu amesema miradi ya umeme vijijini haina fidia, kwa kuwa serikali imempunguzia mwananchi mzigo wa gharama za kuunganishiwa nishati ya umeme kwa kugharamia kwa asilimia mia fedha za ujenzi wa miundombinu pamoja na huduma za kuunganishiwa umeme.

Amesema ili kuhakikisha kwamba adhma ya serikali ya kuunganishia umeme wanawancho wote hasa wa vijijini, ni vyema wananchi wakatoa ushirikiano katika miradi hiyo ikiwemo kutodai fidia.

“Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini inatekeleza mradi huu,  lengo ni kuhakikisha Watanzania zaidi ya asilimia 85 wanatum ia umeme ifikapo 2025. Ili kuhakikisha lengo hili linafikiwa, serikali inagharamia gharama za ujenzi wa miundombinu na gharama ya kufikisha umeme  kwa asilimia 100 na wananchi kulipa sh. 27000 tu ikiwa ni kodi ya VAT,” amesema Mgalu na kuongeza.

“Hivyo miradi ya umeme vijijini haina fidia, natumia fursa hii kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika miradi huu ikiwemo kutodai fidia. Sisi tunaendelea kuelimisha kadri tunapopata fursa, tunawaomba watupe nafasi zaidi.”

Aidha, Mgalu amesema serikali itahakikisha vijiji vilivyopitiwa na msongo mkubwa wa umeme ambavyo havijaunganishiwa umeme, vyote vitaunganishwa na huduma hiyo ifikapo mwezi Desemba 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!