January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kuwapa mitaji wahitimu vyuo vikuu

Spread the love

SERIKALI imesema inaandaa mpango wa kuweza kuwapa mitaji wahitimu ambao wamemaliza vyuo vikuu ambao kwa sasa hawana ajira. Anaandika Danny Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kuwapatia mitaji midogomidogo wahitimu hao serikali inaweka utaratibu wa kuweka rekodi ya wahitimu wote waliohitimu vyuo hivyo na hawana ajira mapaka sasa.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu,) Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM).

Mbunge huyo ametaka kujua ni wahitimu wangapi hawana kazi hadi sasa kutoka elimu ya vyuo vya juu nchini.

Pia alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuta ajira kwa wahitimu au kuwawezesha kujiajiri hasa vijana.

Akijibu maswali hayo Mavunde amesema kwa mwaka 2014 vijana wahitimu wa elimu ya juu wasio na ajira wanakadiriwa kuwa 27,614 ambapo kati yao 14,271 ni wanawake na 13,343 ni wanaume.

Amesema serikali iliendelea na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na suala la ajira kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kuajiriwa au kujiajiri.

Amesema pamoja na kuwepo kwa mikakati mbalimbali lakini bado serikali inatambua kuwepo kwa adha kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana jambo ambalo serikali inatafuta ufumbuzi wa jambo hilo.

error: Content is protected !!