July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kusimamia ruzuku za wachimbaji

Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Spread the love

SERIKALI imesema, itahakikisha inasimamia fedha za ruzuku zinazotolewa kwa wachimbaji wadogo nchini  zinagawiwa kwa uwiano unaofanana. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busanda, Lolensia Bukwimba (CCM).

Akiuliza swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini kunakuwepo na upendeleo wakati wa utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji wadogo.

“Kunamalalamiko kuwa ruzuku ambayo inatolewa kwa wachimbaji wadogo inatofautiana wapo ambao wanapata nyingi na wengine kupata shida wakati wa kutoa ruzuku hiyo,” amehoji Bukwimba.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwatengea maeneo wachimbaji wadogo.

Mwijage amesema serikali inaendelea na utaratibu wa kuwatengea maeneo wachimbaji wadogo ili waweze kufanya shughuli zao kama kawaida.

“Katika mwaka wa fedha 2008/09 serikali ilitenga na kuyagawa maeneo mawili ya uchimbaji mdogo wa dhahabu katika Wilaya ya Geita.

“Maeneo hayo ni Rwangasa (heka 710) na nyarugusu (hekta 510),maeneo hayo yalitengwa baada ya kampuni ya IAMGOLD Tanzania Limited kukubali kuyaachia ili yagawiwe kwa wachimbaji wadogo” alisema.

error: Content is protected !!