Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Biashara Serikali kupunguza kodi kwenye sukari, mafuta
Biashara

Serikali kupunguza kodi kwenye sukari, mafuta

Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itapunguza kodi ya sukari itakayoingizwa nchini kwa hadi asilimia 10 ili kupata unafuu wa bei ya didhaa hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Mwiguli ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 11 Aprili wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa bei nchini.

Amesema mbali na sukari pia wataangalia tozo za Serikali katika nishati ya mafuta ambazo zinaweza kupunguzwa na kazi hiyo itachukua hadi wiki moja kukamilisha.

Pia amesema watakwenda kuangalia kodi katika mafuta ya kula ambapo amesema wameshailekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania kuangalia ndani ya mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu kuweka viwango vipya vya kodi ili kupunguza makali.

“Tutashirikiana na wenzetu wa sekta binafsi ili kuangalia kiwango ambacho kitasaidia wananchi waweze kupumua kwa kupata unafuu wa bei,”

“Kwa maana hiyo tutakuwa tumeshagusa sukari, nishati ya mafuta, mafuta ya kula na kwenye mbolea kama ambavyo Waziri (Dk. Kijaji) ameeleza,” amesema Nchemba.

Vilevile amesema watapunguza sehemu ya gharama zilizokuwa zinaongezeka kwenye usafiri kwa kupunguza gharama kwenye vifaa vya usairishaji ikiwemo semi trela n.k.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini...

BiasharaHabari

NMB yavutia wabunifu suluhisho za kifedha, Dk. Mpango agusia vijana

Spread the love  MFUMO wa majaribio wa suluhishi za kifedha ulioandaliwa na...

BiasharaHabari

NMB Nuru Yangu yazinduliwa, 200 kunufaika

Spread the loveBENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi...

BiasharaHabari

Waziri Bashe uso kwa uso vigogo NMB bungeni

Spread the loveWAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amekutana na kufanya...

error: Content is protected !!