January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kupima maeneo yenye migogoro

Spread the love

WIZARA ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi imeandaa mpango wa kupima maeneo yote ambayo yana migogoro baina ya wananchi na hifadhi nchi nzima katika kipindi cha mwaka 2015/16. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa bungeni mjini hapa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso (Chadema), aliyetaka kujua ni lini serikali itamaliza mgogoro huo utamalizika kati ya wananchi na hifadhi ya Mkongonelo iliyoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

“Hifadhi ya Mkongonelo, wananchi wameuwawa na askari wameuwawa, pale wananchi wanaomba kilomita 50 tu ili mgogoro uishe lakini bado ni tatizo mpaka leo,” amesema.

Katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Paresso (Chadema), alitaka kujua ni lini matokeo ya kamati ya ndogo iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii, kwa ajili ya kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wananchi na hifadhi wa kata ya Bunger na hifadhi ya Taifa ya Manyara.

Pia alitaka kujua ni lini wananchi watapewa taarifa ya kamati hiyo. Akijibu Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Ramo Makani, amesema taarifa ya Tume imebaini kuwa, kwa ujumla chanzo kikubwa cha mogogoro baina ya wananchi na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

“Ni idadi kubwa ya mifugo na kukosekana eneo la kuchungia katika kijiji cha Buger, Tume imependekeza hatua mbalimbali za kuchukuliwa,” amesema.

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na za kuchukuliwa ambazo ni pamoja na kufanya sensa ya mifugo kwa vijiji vilivyopo katika kata ya Buger ili kubaini idadi ya mifugo iliyoko dhidi ya ukubwa wa ardhi waliyonayo.

Nyingine ni vijiji kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, kutoa elimu ya uhifadhi na sheria katika vijiji na kuimarisha zilizopo ili kutelekeza vema majukumu yake.

Aliitaja hatua nyingine kuwa ni Tanapa kuweka nguvu kuchangia miradi ya maendeleo ya maendeleo ya jamii kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi.

Amesema wizara yake itaandaa kikao cha wadau ndani ya miezi mitatu ili kuwasilisha mapendekezo ya kamati na kujadili utekelezaji wake.

error: Content is protected !!