Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali kupiga mnada mamba, viboko
Habari Mchanganyiko

Serikali kupiga mnada mamba, viboko

Mamba
Spread the love

DAKTARI Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii amesema serikali imeamua kuuza asilimia 10 ya mamba wote nchini ili kupunguza changamoto ya wanyama wakali kuvamia maeneo ya watu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Kigwangalla ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 17 Agosti 2019.

Dk. Kigwangalla amesema kwa sasa kuna ongezeko la vitendo vya wanyama wakali kuvamia maeneo ya watu, na kuleta athari kwa wananchi na mali zao. Hivyo hatua ya kuuza wanyama hao itasaidia kupunguza migogoro kati ya wanadamu na wanyamapori.

“Changamoto mpya imezaliwa, wanyama wakali na waharibifu wamezidi na wanavamia maeneo ya watu. Tumeamua kuuza asilimia 10 ya mambo wote nchini,” ameandika Dk. Kigwangalla kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla amesema serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito.

Dk. Kigwnagalla amesema wanyama hao watauzwa kwa njia ya mnada, na kwamba utaratibu wa zoezi hilo utatangazwa kuanzia wiki ijayo.

“Aidha, tutauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito iliyopo mjini, kama vile pale Mpanda, Mafia na Babati. Mauzo ya wanyama hawa yatafanyika kwa njia ya mnada kwa utaratibu ambao utatangazwa wiki ijayo,” amesema Dk. Kigwangalla.

Aidha, Dk. Kigwangalla amesema serikali itaanzisha mradi wa kuweka uzio kwenye maeneo yenye historia ya matukio ya mamba kudhuru watu, ikiwemo Kijiji cha Maleza kilichopo Wilaya ya Songwe mkoani Songwe na Ruvu .

“Sambamba na maamuzi haya, tunaanzisha vituo vya kudumu vya ulinzi kwenye maeneo yote korofi, ambapo wanyama wakali na waharibifu kama Tembo na Simba wamekuwa wakileta shida kwa wananchi. Tutaendelea pia kufundisha wananchi namna ya kujisalimisha kama wakikutana na wanyamapori,” amesema Dk. Kigwangalla

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!