Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali kupanga bei elekezi ya madini
Habari Mchanganyiko

Serikali kupanga bei elekezi ya madini

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula
Spread the love

SERIKALI imesema itapanga bei elekezi ya madini ili kundoa urasimu wanaofanyiwa wachimbaji wadogo wakati wa uuzaji. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alipotembelea kijiji cha Manda kilichopo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo kunachimbwa madini ya jasi (Gypsum).

“Kijiji cha Manda changamoto kubwa ni soko la gypsum, inaonekana wazi wachimbaji wanawaonewa kuna watu wanwalalia. Tumepanga tume tukae pamoja tutengeneze, tuziweke bei elekezi ili wanao nunua madini wafuate bei hizo.

“Sababu watu wetu wamewekeza kwenye madini hayo tumekuta malundo ya Gypsum yako sokoni bei wanayoambiwa watanunua hairidhishi,” alisema Pro. Kikula.

Prof. Kikula aliongeza kuwa “Hiyo hiyo gypsum inanunuliwa Itigi kwenda Mtwara kwa bei ya kutupwa, wananchi wanapata shida wanasafirisha kwa bei ndogo. Tutatengeneza bei elekezi ili iwe kigezo cha ununuzi na uuzaji wa madini sokoni.”

Katika hatua nyingine, Prof. Kikula aliwataka wachimbaji wadogo kuheshimu mamlaka za maeneo wanayochimba madini ikiwa pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa serikali husika ili kuepusha migogoro.

“Katika ziara yetu tumekwenda kujua matatizo ya uchimbaji, tumekwenda Manzase njia ya kutoka Dodoma hadi Iringa kabla ya kuzungumza na wachimbaji tumezungumza na serikali ya kijiji kuhusu uchimbaji.

Wachimbaji lazima waheshimu mamlaka ya maeneo wanayochimba bila ya kuwa na mahusiano mazuri kunaleta migogoro,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!