May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kuongeza watumishi Hospitali za Kanda, Rufaa

Prof, Abel Makubi Mganga mkuu wa Serikali

Spread the love

 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, iko mbioni kuajiri wataalamu 473 wa kada mbalimbali za afya, ambao watapelekwa kuhudumia katika Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa na vyuo vilivyoko chini ya wizara hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 13 Mei 2021, na Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Prof. Makubi amesema watumishi hao watapelekwa katika Hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC). Hospitali ya Kanda ya Mbeya, Bugando na Benjamini Mkapa pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

“Watalaamu 473 chini ya uratibu wa wizara ambao watanufaika na nafasi hizi ni pamoja na; madaktari wauguzi, wafamasia, wateknolojia wa dawa, wateknolojia wa maabara, wateknolojia wa mionzi.
Wateknolojia wa macho, watoa tiba kwa vitendo, maafisa afya mazingira, wasaidizi wa afya, makatibu afya, maafisa ustawi wa jamii na maafisa lishe,” amesema Prof. Makubi.

Mbali na ajira 473, Prof. Mkaubi amesema wataalamu 74 wa kada mbalimbali, wataajiriwa katika Maabara Kuu ya Taifa.

Katibu Mkuu huyo wa Afya amesema ajira hizo) zitajaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali.

error: Content is protected !!