August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kununua ndege nne

Spread the love

SERIKALI imesema, ina mpango wa kununua ndege nne mpya kwa ajili ya usafiri wa abiria, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakati akijibu swali la nyongeza la Joyce Sokombi, Mbunge wa Viti Maalum, (Chadema).

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa ununuzi wa ndege ili kuondokana na adha ya usafiri wa ndege nchini.

Amesema serikali imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya ndege lakini bado kuna tatizo kubwa la usafiri wa ndege kutokana na taifa kuwa na ndege moja.

Awali katika swalili la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua ni lini serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Musoma katika hadhi ya kitaifa kama siyo kimataifa.

Alitaka kuelezwa ni kiasi gani cha fedha kinachopotezwa taifa kutokuwa na ndege zake kwa ajili ya kuleta watalii hapa nchini.

Akijibu maswali hayo Dk. Kalemani amesema kwa sasa taifa lina mpango wa kununua ndege mbili mpya zenye uwezo wa kubeba abiria 78 kila moja.

Amesema licha ya kununua ndege hizo pia serikali itanunua ndege nyingine mbili mpya ambapo moja ina uwezo wa kubeba abilia 120 na nyinine ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 155.

Amesema serikali imekuwa ikifanya matengenezo ya miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Musoma ili kuendelea kutoa huduma kama ilivyokusudiwa wakati wa mpango wa kukijenga kwa hadhi stahiki ikiendelea.

error: Content is protected !!