April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Kuna viwanda vipya 3,000

Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Spread the love

SERIKALI imeeleza kuwa, mpaka sasa kuna jumla ya viwanda vipya 3,000 tangu kuanza kwa kampeni ya ujenzi wa viwanda katika Serikali ya Awamu ya Tano. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 12 Juni 2019 na Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Sophia Mwakagenda.

Mwakagenda alitaka kujua idadi ya viwanda vilivyojengwa tangu kuanza mkakati wa ujenzi wa viwanda 100 kila mkoa. Kwenye swali lake amedai, mkakati huo ulianzishwa kisiasa.

 Waitara amesema,  tayari kwenye mikoa serikali imetenga maeneo kwa ajili ya viwanda ambapo tayari 300 vimeishajengwa.

“Mkakati huu ni sehemu ya mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano, ili kujenga uchumi wa viwanda uliofungamanishwa na maendeleo ya watu,” amesema.

error: Content is protected !!