June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kukamilisha kituo cha Afya cha Chipole

Spread the love

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeahidi kukamilisha ukarabati wa Kituo cha Afya cha Chipole Songea Vijijini kilichoungua moto mwaka 2013. Anaandika Mwandishi Maalum … (endelea).

Kituo cha Afya cha Chipole kinamilikiwa na Shirika la Watawa wa Mtakatifu Agnesi Chipole na inahudumia takribani wakazi 7,434 wa kata hiyo, hivyo kukamilika kwake kutawezesha kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja na uboresha hali za afya za wakazi hao.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa kituo hicho, leo (12 Januari, 2016) Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa, kufuatia kuungua kituo hicho Ofisi ya Waziri Mkuu awali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho.

“Tumekagua ukarabati wa kituo hiki cha afya na tumeona pamoja na kuambiwa na uongozi kuwa pamoja na fedha tulizozitoa lakini bado kuna mahitaji ya msingi yanahitajika ili kiweze kuwahudumia wanakijiji wanaokizunguka. Tunaahidi kukamilisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na maabara” amesema Msuya.

Awali akitoa maelezo ya maendeleo ya ukarabati wa kituo hicho cha afya, Makamu wa Mama Mkubwa wa Chipole, Sairis Mkinga alifafanua kuwa, pamoja na mapungufu ya chumba cha maabara lakini bado kituo hicho cha afya kinao upungufu wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa.

“Tunayo changamoto bado ya kuwa na sehemu maalum ya mapokezi ya wagonjwa na wagonjwa kupokea dawa. Pia panahitajika mahali kwa akina mama wajawazito kujifungulia kwani kwa sasa vyumba hivi viko karibu sana na vyumba vya wanaume lakini tunahitaji chumba maalum kwa aijili ya kliniki ya watoto,” alisisitiza Sista Mkinga.

error: Content is protected !!