June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kujenga majengo ya mahakama

Muonenako wa Mahakama za Tanzania

Spread the love

WIZARA ya Katiba na Sheria ina mpango wa kujenga na kukarabati majengo mbalimbali ya Mahakama nchini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Lupa, (CCM)Victor Mwambalaswa.

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kujenga Mahakama ya wilaya ya Chunya.

Akijibu swali hilo, Mwalimu amesema katika mwaka wa fedha 2015/16, serikali ina mpango wa kujenga na kukarabati majengo mbalimbali ya Mahakama nchini ikiwemo ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Chunya.

Aidha, amesema serikali inatekeleza mpango wa kujenga na kukarabati majengo ya Mahakama nchini kulingana na upatikanaji wa fedha ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Amesema katika mwaka wa fedha 2014/15, serikali ilipanga kujenga Mahakama ya wilaya ya Chunya lakini mradi huo haujatekelezwa kutokana na ukosefu w fedha za miradi ya maendeleo.

error: Content is protected !!