Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali kuja na utaratibu mpya wa kupanga shule bora
Habari za Siasa

Serikali kuja na utaratibu mpya wa kupanga shule bora

Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu
Spread the love

 

HUENDA Serikali nchini Tanzania ikaja na utaratibu mpya wa kupanga shule bora na zile za nafasi za mwisho baada ya kufutilia mbali utaratibu uliokuwepo awali wa kuangalia matokeo ya mtihani wa mwisho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa bungeni leo jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, wakati akitoa ufafanuzi wa sababu ya Baraza la Taifa la Mitihani kuachana na utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora.

Profesa Mkenda amesema njia iliyokuwa ikitumia kupanga shule bora kwa kuangalia matokeo ya mwisho imepitwa na wakati na nchi nyingi duniani zimeachana nayo.

Amesema sababu ya kuachana na njia hiyo ni utata wa namna ya kutathimini shule bora, “chukua kwa mfano shule yenye wanafunzi 1oo waliomaliza kidato cha nyingine ina wanafunzi 20. Ile ya wanafunzi 100 wanafunzi 70 wamepata A na wanafunzi 30 hawakupata A, yenye wanafuzni 20 wote wamepata A. Kwa kuangalia wastani wa ufaulu ni wazi kuwa shule yenye wanafuzni 20 itatangazwa kuwa ni shule bora kuliko yenye wanafuzni 100, wengine watasema shule yenye wanafunzi 70 wakapata A ni bora kuliko shule yenye wanafunzi 20,”amesema Mkenda.

Amesema mbali na utata huo hiyo ya tathimini huweka shinikisho kwa shule kufanya namna ya kuondoa wanafaunzi ambao hawana uwezo wa kupata A ili iweze kuwa shule bora.

“Wewe mzazi ungetaka nini mwanao ameingia shuleni alikuwa nafaulu vizuri amefika kidato cha tatu ameugua au amepata nini hafanyi vizuri sana ungetaka shule hiyo imwondoe ili iwe na wastani mzuri au iwekeze kumsomesha huyo mtoto ili afanye vizuri,” amehoji Mkenda.

Akitoa ufafanuzi zaidi amesema zipo njia tatu duniani za kupanga ubora wa shule ikiwemo ya kuangalia matokeo ya mwisho zingine zikiwa ni kuangalia thamani iliyoongezwa kwa mwanafunzi (Value addition) na ya kuangalia mazingira ya shule katika kuongeza thamani kwa mwanafunzi (Conceptual Value Addition).

Amesema njia ya value addition (kuongeza thamani), mwanafunzi inaangalia mwanafunzi alipoingia alikuwaje na alipomaliza alikuwaje.

“Maana yake shule imechangia nini kumwendeleza yule mwanafunzi, njia hii inatumika na Uingereza sasa hivi nimesoma Uganda nao wanatumia wakitaka kufanya tathimini wataangalia yule mwanafunzi alipoingia alikuwaje na alivyoondoka alikuwaje,” amesema Mkenda na kuongeza;

“Maana yake shule ambayo inaweza kuwa bora inaweza kuwa shule ya kata ambayo imechukua wanafuzni wa wastani tu lakini baada ya kumaliza wakawa bora kuliko shule ambayo inachukua wale bora tu hata kama haifundishi vizuri sana wale wanafunzi wanavipaji ni bora sana wakamaliza wote wakapata A.”

“Tukiweza kufanya hivyo tukakusanya hizi takwimu tunaweza kuliambia Baraza lifanye ranking lakini kwa kutumia njia hii,” amesema.

Amesema njia ya tatu ambayo ni bora zaidi ni ile inayoangaliaa sio tu yule mtoto aliingiaje shuleni alikuwaje lakini mazingira yake yakoje.

“Mfano shule ipo mazingira ambayo ni magumu sana, maji hayapatikani kwa karibu, hamna mabweni, jamii ni maskini sana, walimu wakafanya kazi kufa na kupona mwanafunzi ameingia wastani lakini akamaliza na A shule hii imeongeza kitu kikubwa zaidi,” amesema.

Haa hivyo amesema njia hiyo inahitaji wataalamu wa takwimu kuzingatia si tu hali ya mwanafunzi bali na mazingira ya ile shule.

“Kwahiyo baraza limeamua halichuki lenyewe jukumu la kutangaza shule bora kwasababu likitangaza shule bora linaambia wazazi hii ndiyo shule bora sasa tunadhani kama mwanao hajaenda kule hajaweza kupata shule bora.

“Tutakapopata value addition approach tutaweza tukasema shule hii pamoja na kuchukua wanafunzi wa wastani inaweza ikawageuza wanafunzi wakafanya vizuri zaidi kwahiyo kama una mwanao unaweza kumpeleka shule hii,” ameongeza.

Aidha amesisitiza kuwa Baraza halijazuia mtu yeyote kusema shule bora ni ipi kwa kuangalia matokeo ambayo yapo wazi kwenye mtandao “sio siri lakini serikali kupitia baraza halichukui jukumu hilo lakini mbele litaangalia namna nzuri ya kurank hizi shule.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!