Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali kuiwezesha DMI majengo, vifaa vya kisasa
Habari Mchanganyiko

Serikali kuiwezesha DMI majengo, vifaa vya kisasa

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete
Spread the love

 

SERIKALI imeahidi kukiwezesha Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI) kwa miundombinu bora na vifaa vya kisasa vya kufundishia ili kiweze kuwa na viwango vya kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ahadi hiyo ilitolewa jana Jumanne tarehe 21 Juni, 2022 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, wakati akifungua kongamano la kwanza la uchumi wa buluu.

Kongamano hilo lililoandaliwa na DMI ni la kwanza kufanyika nchini kuhusu uchumi wa buluu na maudhui yake ni ‘Kuibua fursa zitokanazo na bahari kwa maendeleo ya taifa’.

Amesema eneo kilipo chuo hicho kwa sasa ni dogo hivyo serikali inaangalia uwezekano wa kutenga eneo kubwa kwenye Mkoa wa Pwani kwaajili ya kupanua shughuli za chuo hicho.

Amesema kwa kuanza serikali imeshatenga Sh bilioni moja kwaajili ya ununuzi wa mfumo wa kufundishia na nahodha wa meli inayofahamika kama Simulators.

“Niliwahi kutembelea hiki chuo hivi karibuni na kwa kweli nilijionea mwenyewe miundombinu ilivyo chakavu lakini mkakati uliopo ni kukiwezesha kuwa cha kisasa na kitakuwa na majengo yenye viwango na kwa kuwa wana maeneo makubwa Mkoa wa Pwani itakuwa kazi rahisi kwetu ,” amesema Mwakibete

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya DMI, Ernest Bupamba, ameiomba serikali iiangalie DMI kwa “jicho la huruma” ikizingatiwa kuwa ndicho chuo pekee kinachotoa mafunzo ya bahari hapa nchini.

Amesema chuo hicho ndicho pekee kinazalisha rasilimali watu inayohitajika kwenye uendeshaji wa uchumi wa buluu hivyo iwapo kitawezeshwa kwa vifaa na majengo kitatoa mchango mkubwa kwenye kufikia malengo yaliyowekwa kwenye uchumi huo.

Ameishukuru Serikali ya visiwa vya Shelisheli kwa namna ambavyo imeisaidia Tanzania katika kupambana na vitendo vya uvuvi haramu kwenye bahari yake.

Amesema mara kadhaa viongozi wa serikali hiyo wamekuwa wakiwasiliana na serikali ya Tanzania kila wanapoona wavuvi haramu na ksiha vyombo vya usalama kwenda kuwakamata na kuwafikisha kunakohusika kwa hatua za kisheria.

“Ni mara nyingi sana Sheli sheli imekua msaada mkubwa kwa Tanzania kwa sababu kule watu wamekuwa wakijaribu kuendesha uvuvi haramu lakini kila wakijaribu wanatupigia simu na serikali inachukua hatua haraka sana na imesaidia kwa kiasi kikubwa,” amesema.

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Tumaini Gurumo amesema kwa mwaka wanazalisha mabaharia 100 ambao wanakidhi soko la ndani na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

“Soko la mabaharia ni kubwa sana sisi tunazalisha 100 kwa mwaka ambao wanakidhi mahitaji ya ndani na wengine wanakwenda kufanyakazi nje ya nchi, vijana wachangamkie fursa hii kwasababu inafedha za kutosha na ajira yake siyo ya kuhangaika,” amesema Dk. Tumaini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!