January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kugawa mbegu kukabili maafa Mungere

Spread the love

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa itatoa mbegu bure za miti ili kukabili maafa ya upepo mkali kwa wakazi 3,000 wa Kijiji cha Mungere. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Wananchi hao ni wale ambao mashamba yao ya migomba yalikumbwa na maafa ya upepo mkali uliosababisha ekari 250 kati ya ekari 300 za mashamba hayo kuathiriwa na upepo huo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua athari za maafa hayo katika Kijiji cha Mungere, Monduli jana, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa, serikali imeamua kuwagawia bure mbegu za miti itakayopandwa kwa kuzunguka mashamba yao ili waweze kukabili maafa hayo ya asili.

“Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu Maafa inalojukumu la kuratibu shughuli za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya kawaida pindi maafa yanapotokea kwa hapa kijijini Mungere tumeamua kukabili maafa yatokanayo na upepo kwa kuwapa wakulima wa zao la ndizi waweze kuipanda miti hiyo itakayowezesha kupunguza kasi ya upepo mkali ambao husababisha migomba kuanguka katika mashamba yao.” amesema Brig. Jen. Msuya

Msuya aliongeza kuwa, idara yake itatoa chakula cha msaada kwa waathirika wa maafa hayo ili waweze kuwa na chakula cha kutumia wakati baadhi ya migomba yao iliyoathirika ikiendelea kuchipuka na mingine kukomaa ambapo wataweza kupata chakula lakini pia na kujipatia fedha kwa kuuza zao hilo.

Awali akizungumza katika ziara hiyo kiongozi wa mila, Alaigwanani Saibulu Olemariki amefafanua kuwa upandaji miti ndio njia pekee ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la ndizi kuweza kukabili maafa ya upepo katika kijiji hicho kwa kuwa mashamba yao yamekuwa yakikumbwa na maafa ya upepo mkali ambao umekuwa ukiangusha migomba ambayo tayari inakuwa imeshabeba ndizi kubwa na zilizo komaa.

“Kama kiongozi wa kimila nitawahamasisha wanakijiji wenzangu hasa wakulima wa mashamba ya migomba kuhakikisha kuwa kila mtu anazungusha miti ya kutosha katika shamba lake lakini pia kuhakikisha kuwa miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji na kutokatwa ovyo,” amesema Olemariki.

Olemariki ameeleza masuala yanayo kuwa kikwazo kwa wakulima hao kuwa ni miundo mbinu ya barabara na umwagiliaji kwa kueleza kuwa pamoja na kijiji hicho kuwa na maafa ya upepo ambayo huathiri mashamba yao ya migomba lakini pia miundombinu ya barabara imekuwa kikwazo cha wakulima hao kwa kushindwa kusafirisha ndizi ili waweze kulifikia soko kwa wakati .

“Tunaomba serikali iweze kuiboresha barabara inayokuja kijijini hapa ili kuweza kuhamasisha wafanyabiashara wengi kufika kijijini hapa kununua ndizi,” amesema na kuongeza:

“Kama tunakuwa hatujapatwa na maafa tunaouwezo wa kuzalisha ndizi nying na hili niombe serikali kuwa sisi tunazalisha ndizi nyingi amabazo tukijengewa mazingira mazuri ya kilimo chetu ikiwa ni pamoja na kujengewa mfereji bora wa maji tunao uwezo wa kuilisha Monduli nzima na hata nje ya hapo,” amesisitiza Olemariki.

 

error: Content is protected !!