July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kuanzisha mradi umaliziaji maboma yaliyoanzishwa na wananchi

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, itaandaa mradi wa kumalizia maboma yaliyoanza kujengwa na wananchi, ikiwemo ya madarasa na zahanati. Anaripoti Bupe Mwakiteleko, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 18 Mei 2022, katika halfa ya uzinduzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda, iliyofanyika mkoani Tabora na kurushwa mbashara katika vyombo vya habari.

Kiongozi huyo wa Tanzania, ametoa ahadi hiyo baada ya uongozi wa Mkoa wa Tabora, kuiomba Serikali yake imalizie maboma takribani 120 ya madarasa, yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na kuishia kati.

“Bajeti ya TAMISEMI kwa kiwango kikubwa itaenda kukamilisha maboma haya ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi. Lakini pia tunajitahidi kuwa na mradi kupitia TAMISEMI, kwenda kumalizia maboma ya zahanati ambayo tayari wananchi wameonesha nguvu zao,”amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!