April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kuamua hatma ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sambamba na Bodi ya Ligi imesema kuwa hatma ya kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara sambamba na Ligi daraja la Kwanza (TPL) inategemea uamuzi wa serikali ambayo itaelekeza muda muafaka wa kuendelea na mashindano hayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa ndani ya Shirikisho hilo imeeleza kuwa Bodi ya Ligi na TFF bado ipo kwenye mchakato wa kujadili namna ya kuendelea na michezo iliyosalia ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, licha ya kutofikia maamuzi lakini jambo hilo litategea zaidi maamuzi ya Serikali.

Ikumbukwe agizo la kusimamishwa kwa Ligi hiyo lilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa tarehe 17 Machi, 2020 baaada ya kutoa tamko la kusimamisha shughuli zote za michezo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababisha na kirusi aina ya corona.

Ligi hiyo ambayo mpaka sasa imebakisha michezo 10 kwa baadhi ya timu ili iweze kukamilika huku klabu ya Simba ikiwa imejikita kileleni kwenye msimamo baada ya kukusanya alama 71 ikiwa imecheza michezo 28

error: Content is protected !!