July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Kima cha chini 100,000 wafanyakazi majumbani

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt Makongoro Mahanga

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, wafanyakazi wote wa majumbani wanatakiwa kulipwa mshahara wa kima cha chini kisichopungua Sh. 100,000. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohammed (CUF).

Mbunge huyo aliihoji serikali na kutaka itoe kauli kuwa, ni kiasi gani cha mishahara ambacho wanatakiwa kulipwa wafanyakazi wa majumbani licha ya wafanyakazi hao kunyanyaswa na waajiri wao.

“Najua kila mmoja hapa ana mfanyakazi wa nadani lakini wafanyakazi hao wamekuwa wakinyanyaswa na wakati mwingine kulipwa mishahara kidogo.

“Sasa naitaka serikali ieleze, wafanyakazi hao wanatakiwa kulipwa kiwango gani cha mshahara kwa mwezi,” amehoji Mbarouk.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Kuruthum Mchuchuli (CUF) alitaka kujua serikali itapeleka lini mkataba Na 189 bungeni unaohusu kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani ili uridhiwe na Bunge.

Akijibu maswali hayo Makongoro amesema, wafanayakazi wote wa nadani wanatakiwa kulipwa mshahara wa Sh. 100,000 kwa mwenzi kama kiwango cha chini cha mshahara.

Makongoro amesema, wafanyakazi wa ndani wanatakiwa kutoa taarifa pale ambapo wanakuwa wanaonewa au kunyanyaswa.

Amesema, pamoja na mchakato huo wa kuridhia mkataba Na 189 unawahusisha wafanyakazi wa majumbani “wafanyakazi hawa kama walivyo wafanyakazi wengine, wote wanaendelea kulindwa na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na 6 ya mwaka 2004.”

error: Content is protected !!