Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali ya Tanzania: Kila mtu alimiliki mil 2.5 mwaka 2019
Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Tanzania: Kila mtu alimiliki mil 2.5 mwaka 2019

Spread the love

SERIKALI imesema, mwaka jana (2019) pato la taifa kwa mtu mmoja mmoja lilikuwa Sh. 2,577,967 kutoka Sh. 2,452,406 mwaka 2018, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 5.1. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Na kwamba, kiasi hicho cha pato la wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2019, ni sawa na Dola za Marekani 1,126.4 ikilinganishwa na Dola za Marekani 1,083.2 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 4.0. 3.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 11 Juni 2020 na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Uchumi wakati akieleza hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019 bungeni jijini Dodoma.

“Aidha, mwaka 2019, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu 54,265,158 ambapo pato la wastani la kila mtu lilifikia shilingi 2,577,967 kutoka shilingi 2 2,452,406 mwaka 2018, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 5.1,” amesema Dk. Mpango.

Amesema, pato la Taifa kwa mwaka 2019 limekuwa kwa asilimia 7.0 kama ilivyokuwa katika mwaka wa fedha wa 2018.

Ukuaji huu ulitokana na kuendelea kuimarika kwa sekta ya madini, kuboreshwa kwa huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege, miradi ya nishati ya umeme, ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya.

“Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji mwaka 2019 ni madini iliyokua kwa asilimia 17.7, ujenzi (asilimia 14.8), sanaa na burudani (asilimia 11.2) na usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 8.7),” amesema.

Pato la Taifa kwa bei za mwaka husika lilikuwa shilingi 139,893,804 mwaka 2019 ikilinganishwa na shilingi 129,043,901 mwaka 2018.

Na kwamba, mwaka 2019, shughuli za kiuchumi za kilimo ambazo zinajumuisha kilimo cha mazao, mifugo, misitu na uvuvi, zilikua kwa asilimia 4.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.4 mwaka 2018.

“Kasi ndogo ya ukuaji ilitokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopelekea kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo. Shughuli ndogo za uzalishaji mazao zilikua kwa asilimia 4.4 mwaka 2019 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.2 mwaka 2018 na zilichangia asilimia 14.8 katika Pato la Taifa mwaka 2019.

“Kiwango cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi za mifugo kilikuwa asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 4.9 mwaka 2018 na zilichangia asilimia 7.4 katika Pato la Taifa mwaka 2019,” amesema Dk. Mpango.

Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mpango

Amesema, kiwango cha ukuaji wa shughuli za misitu na uvuvi kilipungua kufikia asilimia 4.8 na 1.5 mwaka 2019, kutoka asilimia 4.9 na 9.2 mwaka 2018. Na kwamba, mchango katika pato la Taifa umebaki asilimia 2.7 na 1.7 mtawalia mwaka 2019 kama ilivyokuwa mwaka 2018. 4.

Shughuli za kilimo sehemu inayouzika zilikua kwa asilimia 4.4 mwaka 2019 wakati sehemu isiyouzika ilikua kwa asilimia 4.6 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.4 na 6.4 mwaka 2018 mtawalia.

Amesema, kiwango cha ukuaji wa shughuli ndogo za kiuchumi za uvuvi, misitu na mazao sehemu inayouzika kilipungua kufikia asilimia 1.5, asilimia 4.8 na asilimia 4.4 mwaka 2019 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 9.2, asilimia 5.2 na asilimia 5.6 mwaka 2018 mtawalia.

“Kasi ya ukuaji kwa shughuli ndogo za kiuchumi za mifugo sehemu inayouzika iliongezeka na kuwa asilimia 5.0 mwaka 2019 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2018.

“Kwa upande wa sehemu isiyouzika, shughuli ndogo za kiuchumi za mazao na misitu zilikua kwa asilimia 4.4 na asilimia 4.8 mwaka 2019 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.1 na asilimia 1.7 mwaka 2018 mtawalia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!