May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: JPM atakuwa mkali zaidi

Rais John Magufuli

Spread the love

 

WATUMISHI wa serikali na wale wanaopewa kazi na serikali, wametakiwa kuzifanya kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa, Rais John Magufuli atakuwa mkali zaidi dhidi ya wazembe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 31 Januari 2021, jijini Dodoma, Dk. Hassan Abbas ambaye ni Msemaji wa Serikali amesema, kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake.

“…kwenye hii mitano tena, atakuwa mkali mara mbili zaidi alivyokuwa mwanzo. Watu watimize wajibu wao kwenye kutekeleza miradhi hii ya serikali,” amesema Dk. Abbas.

Amesema, Rais Magufuli amekuwa kwenye ziara Kanda ya Ziwa na kwamba, ujumbe wake mkuu ilikuwa ni wananchi kulipa kodi pamoja na amani ya nchi.

“Katika ziara zote hizi amesisitiza amani, kulipa kodi na mambo ya kukwepakwepa kulipa kodi hayatosaidia, pia usimamiizi imara wa miradi.

“Watu wafanye kazi. Kule Misenyi mliona mtiti waliopata wale wakandarasi wa maji. Nitumie fursa hii kuwasisitiza watendaji wote wa serikali lakini wakandarasi na wote ambao wamepewa miradi kwa lugha aliyotumia mwenyewe imejitosheleza, kwenye hii mitano tena atakuwa mkali mbili zaidi,” amesema.

error: Content is protected !!