July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Serikali iwekeze katika sekta ya maji’

Adha ya ukosefu wa maji nchini

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuwekeza katika sekta ya maji ili kuondoa changamoto zinazotokana na ukosefu wa maji safi na salama. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISIOnline leo jijini Dar es Salaam, Gemma Akilimali- Mwanaharakati na mchambuzi wa masuala ya bajeti amesema “licha ya kuwepo kwa juhudi za kukabiliana na kero ya maji, lakini serekali bado haijafanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya maji”.

Gemma amesema, juhudi zinazofanywa na serikali ni za kupunguza tatizo kwa muda mfupi. Hasa katika kipindi hichi cha “wiki ya maji” fedha nyingi zinatumika katika maonesho na sherehe badala ya kutafakari ni namna gani ya kuhakikisha kero ya maji inamalizika.

“Tanzania tuna vyanzo vingi vya maji, lakini maji mengi hasa ya mto Rufiji yanapotea bahari. Hakuna uwekezaji wa miondombinu kuhakikisha maji haya yanawafikia wananchi,” amesema Gemma.

Aidha, Gemma anahoji “ni namna gani sekta binafsi imefanikiwa kusambaza maji ya viwandani (maji ya chupa) yenye gharama kubwa nchini kote wakati serikali imeshidwa kusambaza maji kwa wananchi?”

Gemma amesema, mbali serikali kushidwa kuwekeza katika sekta ya maji, pia changamoto nyingine zinazosababisha ukosefu wa maji safi na salama ni ufinyu wa bajeti ya maji na mabadiliko ya hai ya hewa yanayoathiriwa na shughuli zinazofanywa na binadamu zikiwemo uchafuzi wa mazingira na kujenga katika vyanzo vya maji.

error: Content is protected !!