January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali isihamishe watu ovyo- Asasi

Baadhi ya nyumba zilizokubwa na mafuriko jijini Dar es Salaam

Spread the love

MTANDAO wa Asasi za kiraia na maendeleo (Policy Forum) kwa kushirikiana na wataalamu wa ushauri na maendeleo, wamekutana kuandaa sera ya kuishawishi Serikali iwafikirie waathirika wa mafuriko na watu wanaoondolewa katika makazi yao kwa shughuli za kiserikali bila malipo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Wataalam hao wa maendeleo nchini ni International Development Consultants (IDC) na Director Center for Community Initiative (CCI).

Kwa mujibu wa asasi hizo, wamefanya utafiti kwa muda mrefu katika manispaa zote za Dar es Salaam na kugundua matatizo yanayowakabiri wakazi wanaoishi mabondeni na maeneo ambayo hayakupimwa na yasiyopaswa kujegwa.

Akizungumza na MwanaHALISIOnline, mmoja washauri hao wa kimataifa, Ibrahim Mwenda, amesema Serikali inatakiwa kushirikiana na taasisi za utafiti na maendeleo nchini ili kubaini changamoto zinazowakabili wananchi.

Mwenda amesema kuwa, imefika wakati serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi itengeneze sera ya uhamishaji na iwatumie washauri mbalimbali ambao watasaidia kutoa elimu juu ya madhara na usalama wa makazi ya raia nchini.

“Huwezi kumwambia tu mtu ahame kwenye makazi yake, kwani sio wote wenye uelewa wa kutosha juu ya ardhi anayoishi, na je unapomwambia ahame unampeleka wapi? Sawa serikali imetenga maeneo maalumu kwa ajili wa watu hao, lakini yanatosha? Amehoji Mwenda.

Kwa mujibu wa Mwenda, taasisi za utafiti na maendeleo zipo tayari kufanya kazi na serikali, isipokuwa serikali bado haiana ushirikiano wa kutosha.”

Endapo serikali itatoa ushirikiano wa kutosha, kuweza kuandaa mikutano na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo hatarishi, hapatakuwa tena na vifo vya makusudi wala kusumbuana na wananchi, kwa kuwa tayari watakuwa na uelewa wa kutosha  juu ya makazi yao,”amesema.

Naye, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Feliciani Komu amesema, serikali pia inaweza kuwa sababu ya matatizo haya ya ardhi, kwa sababu hakuna utaratibu wa kupima ardhi na kuiweka katika uangalizi maalumu.

“Inabidi serikali iungane na taasisi binafsi kama hizi ili ijue ni namna gani ya kuwashauri, na iangalie jinsi gani ya kuwaondoa wasiwakurupushe kwa sababu tangu mtu anapoanza kujenga serikali inaangalia tu,”amesema Komo.

error: Content is protected !!