July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ingepanua kwanza magereza

Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania

Spread the love

MKUTANO wa 19 wa Bunge la Jamhuri umemalizika mkoani Dodoma. Pamoja na mengine, umepitisha “Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni.”

Katika Bunge hili, serikali ilipeleka miswada zaidi ya mitano chini ya hati ya dharura. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuwasilisha lundo la miswada kwa waakati mmoja, tena kwa kutumia utaratibu wa hatia ya dharura.

Ndani ya miswada hii, kumejazwa vifungu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.

Muswada wa sheria ya makosa ya mtandao unaainisha makosa ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Inaweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na mengineyo.

Muswada wa sheria ya Takwimu (mwaka 2013), ni muswada wa sheria ya kufuta sheria ya Takwimu, kuanzisha ofisi ya taifa ya Takwimu; Bodi ya usimamizi wa takwimu, na kuweka masharti yanayohusu uratibu wa mfumo wa Kitaifa wa Takwimu.

Kitendo cha kupeleka miswada bungeni bila kushirikisha wadau, ni dalili tosha kuwa sheria hizi hazikutungwa ili kusaidia taifa. Zimetungwa ili kuminya uhuru wa wananchi wa kujieleza na kupata habari.

Kwa mfano, muswada wa sheria ya Takwimu, malengo yake siyo kuratibu takwimu za kitaifa tu; muswada umeitambua ofisi ya taifa ya takwimu kama kitovu kikuu cha utoaji wa takwimu nchini.

Hii maana yake ni kwamba taasisi zote za serikali, mashirika binafsi, taasisi za elimu ya juu, vyuo vikuu na watu binafsi, hazitokuwa na uhuru wa kutoa matokeo ya tafiti wanazozifanya bila ya kibali au ridhaa ya serikali – ofisi ya takwimu.

Sheria hii mpya imezitaja taarifa na takwimu zote nchini, zikiwamo zile zilizoandaliwa na taasisi binafsi na kuziingiza katika mfumo wa kitaifa wa takwimu unaoratibiwa na ofisi ya takwimu. Hili halikubali na kamwe haliwezi kufanyika katika nchi inayodai kuwa ina uhuru na kuheshimu haki ya watu kujieleza.

Aisha, kwa mujibu wa sheria hii, tasisi zote zikiwemo binafsi zinapaswa kuwajibika ofisi ya takwimu na kupata ridhaa ya mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Takwimu ili kutoa taarifa zake za kitakwimu.

Kifungu cha 20 (2) kinasema, “Takwimu zote zitakazotolewa na wakala – taasisi binafsi, mashiirika ya utafiti, wadau wa maendeleo, watumiaji au wazalishaji wengine wa takwimu – zinapaswa kukidhi matakwa ya ofisi ya takwimu na kuidhinishwa na mkurugenzi mkuu.”

Sheria inatoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia ya makosa yalianishwa katika sehemu ya tatu ya sheria.

Kwa mfano, kifungu cha 37 cha sheria hiyo kinasema mtu yoyote au tasisi itakayotoa takwimu au taarifa za kitafiti ambazo ofisi ya takwimu inaziona ni za uongo, anatenda kosa na kustahili kifungo cha miezi sita na faini isiyopungua Sh. 2 millioni.

Hii maana yake ni kuwa tafiti zote zinazofanyika, ni lazima zisimamiwe na kupitia ofisi ya Takwimu. Kuna tofauti kubwa kati ya chapisho ka Kiswahili na kile la Kingereza katika sheria hii. Hata adhabu zilizoainishwa zinatofautiana.

Hali ni hiyo hiyo katika sheria ya “makosa ya mitandao.” Sheria hii imeletwa kwa nia mbaya. Inabinya kwa kiasi kikubwa uhuru wa wananchi kuwasiliana na kupashana habari. Imelenga kufuta kabisa matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, twitter, blogu na mengineyo.

Kupitishwa kwa sheria hii katika muktadha wa sasa, kutasabisha watu wengi kuwekwa kizuizini bila sababu za msingi. Sheria imetungwa kwa uharaka na kwa malengo yaliyojificha. Yawezekana imeandaliwa maalum katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, ili kusaidia wizi wa kura. Jambo hili halikubali na nilazima tulipinge.

Hivyo basi, ni muhimu Rais Jakaya Kikwete asiruhusu sheria hizi kutumika kwa maslahi ya taifa na watu wake.

Vingenevyo, kama anataka kusaini na kuwa sheria, basi aanze na kupanua magereza ili yaweze kuwa na uwezo wa kuhifadhi watu watakaopatikana na hatia. Wakosaji watakuwa wengi, hata rais mwenyewe anaweza kuwamo.

error: Content is protected !!