Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali inaweka nguvu kwenye TEHAMA-Prof. Ndalichako
Elimu

Serikali inaweka nguvu kwenye TEHAMA-Prof. Ndalichako

Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu
Spread the love

PROFESA Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoljia amesema, serikali inatambua umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya teknolojia ya habari na wasiliano (Tehama), ili kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Oktoba 2019, jijini Dodoma wakati akifungua Kongomano la Nne la Mtandao Jamii katika nchi za Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Amesema, kwa dunia ya leo Tehama ni jambo lisilokwepeka katika kuwezesha jamii kuzifikia fursa mbalimbali.

“Mawasiliano ni nyenzo muhimu, serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuimarisha mawasailiano kwa wote, hadi kule ambako bado wananchi hawajafikiwa hasa vijijini,” amesema.

“Nawaombeni mtumie kongamnao hili pia katika kutathimini ukuaji wa mawasiliano nchini, baraani Afrika lakini pia dunia kwa ujumla ili kuweza kuona ni vipi tunaweza kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa kwa haraka,” amesema Prof. Ndalichako.

Prof. Faustne Bee, Makamu Mkuu wa UDSM amesema, mkutano huo umehusisha washiriki kutoka katika maeneo mbalimbali duniani.

Na kwamba, kongamano hilo ni la nne na Tanzania imepewa wenyeji mwaka huu ambapo washiriki kutoka Kenya, Uganda, Cameroon, Liberia, Ghana na Uhispiania wanashiriki.

Amesema, lengo la kongamano hilo ni kupeleka huduma kwa jamii kupitia mfumo wa mawimbo ya Televisheni na kuzifikia taasisi zote za serikali, zikiwemo shule katika maeneo yasiyofikiwa na huduma ya internet ifikapo 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Watakaopata Division One St Anne Marie Academy kupewa iphone ya macho matatu

Spread the loveMkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson...

Elimu

Prof. Muhongo apinga TAMISEMI kusimamia elimu

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameshauri masuala...

Elimu

SUA kuboresha ufundishaji kupambania ajira za wahitimu

Spread the love  CHUO kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani hapa...

Elimu

Wanakijiji waamua kujenga sekondari, wamuangukia Rais Samia

Spread the love  WANANCHI wa Kijiji cha Wanyere, Wilaya ya Musoma Vijijini...

error: Content is protected !!