January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Serikali inapenda wanyama kuliko binadamu’

Tembo wakiwa mbugani

Spread the love

MBUNGE wa Mchinga, Saidi Mtanda (CCM), amesema Wizara ya Malisili na Utalii inapenda wanyama pori kuliko binadamu wa Mchinga. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Katika swali lake bungeni leo, Mtanda amehooji, “…kwa sasa wananchi wa Mchinga wameniambia kuwa wakati wa kuomba kura twende tukaombe kwa wanyama kwa kuwa ndio wanapendwa zaidi ya binadamu.”

“Haiwezekani sisi mazao yetu yanashambuliwa na Tembo wakati huo hatupati fidia ya uharibifu na hapohapo tunafukuzwa katika maeneo kwa madai kuwa ni hifadhi ya wanyama pori,” amesema.

Swali la Mtanda lilitokana na swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema), aliyetaka kujua ni lini kanuni za Maliasili za mwaka 2011 za kulipia fidia zitarekebishwa.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammood Mgimwa, amesema kuwa sio kweli kuwa wizara inawapenda wanyama kuliko wapiga kura wake.

Hata hivyo, amesema sekta ya utalii inaliingizia taifa pato la asilimia 19 kwa mwaka, hivyo ni vyema pia kuwalinda na kuwatunza wanyama nchini.

Kuhusu suala la uandikaji wa Kanuni, amesema kwa sasa kanuni 11 zimekamilika na kanuni 7 zipo katika hatua mbalimbali.

error: Content is protected !!