Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali imeweka mikakati kukabiliana na ukatili wa kijinsia- Msigwa
Habari Mchanganyiko

Serikali imeweka mikakati kukabiliana na ukatili wa kijinsia- Msigwa

Spread the love

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia hususan kwa Wanawake kwenye maeneo mbalimbali nchini, ikiwepo kuanzisha Wizara maalum ya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambayo imekuwa kinara kushughulikia changamoto hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema ukatili dhidi ya wanawake ni jambo ambalo halikubaliki mahali popote ikiwepo kwenye vyumba vya habari na hivyo Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali, kuhakikisha kunakuwa na kampeni za kukabiliana  na hali hiyo hususan kwenye mitandao ya kijamii ambako kumekuwa na udhalilishaji wa kundi hilo.

Aliyasema hayo jana tarehe 18 Septemba 2023 katika mkutano wa Wabunge na Wadau wa Sekta ya Habari uliohusu kukabiliana na ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii na hasa Wanawake uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Ukatili dhidi ya Wanawake iwe kwenye vyombo vya habari, iwe kwenye jamii, iwe mahali pengine popote haukubaliki, na Serikali imekuwa ikishirikiana na Wadau kuhakikisha kwamba kunakuwa na kampeni mbalimbali za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake, na sasa hivi kumeanza kuja kwa kasi sana ukatili unaofanywa dhidi ya wanawake kwenye mitandao ya kijamii, kwenye majukwaa ya mitandaoni, hili ni jambo ambalo halikubaliki” amesema Msigwa.

Kuhusiana ukatili wa Wanawake kwenye vyombo vya Habari, Msigwa anasema Serikali inakamilisha kanuni zitakazoleta usawa wa kijinsia kwenye vyombo hivyo.

“Kwa upande wa vyombo vya habari, tunayo sheria yetu ya huduma za habari ambayo tumeifanyia marekebisho hivi karibuni, na sasa Waziri anakamilisha kanuni, kwenye zile kanuni moja ya maeneo ambayo tunakwenda kuangalia ni namna gani ambavyo tutaongeza idadi ya wanawake kwenye vyombo vya habari, kwenye vyumba vya uhariri, wawepo wa kutosha, lakini pia tunakwenda kuangalia ni namna gani kanuni zetu zimechukua hatua dhidi ya vitendo hivyo ambavyo pia kwenye vyombo vya habari vinajitokeza” amesema Msigwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira amesema ni lazima jamii na watumiaji wa mitandao wajengewe uelewa ili kuepukana na ukatili huo pamoja na kuwa na sheria ambazo zinalinda kila mtu kuweza kushiriki katika mitandao kwa usawa.

“Ni lazima tufanye kampeni ya kitaifa , ni lazima tujenge uelewa wa wadau, kujenga uelewa wa watumiaji wa mitandao ya kijamii lakini pia kuweka sheria ambazo zinalinda kila mtu kuweza kushiriki katika mitandao kwa usawa, na tumeshaambiwa kwamba Serikali italeta Bungeni Sheria ya vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi, kwa hiyo na sisi tujitajipanga kuchangia ipasavyo katika maeneo hayo ili sheria hizo pia zitambue ukatili wa jinsia katika mitandaio ya kijamii,” amesema Lugangira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

Habari Mchanganyiko

MAIPAC kusaidia Kompyuta shule ya Arusha Alliance

Spread the loveTaasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) imeahidi...

error: Content is protected !!