July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Serikali imeshindwa kuboresha maisha ya wananchi’

Wanakijiji wakichota maji

Spread the love

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mpwapwa, Alexander Nyaulingo amesema hakubaliani na sera ya serikali ya utunzaji wa mazingira kwani serikali imeshindwa kuwaboresha maisha ya wananchi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Amesema  kama wananchi hawataweza kuboreshewa maisha na kuondokana na umasikini uliokithiri basi kauli ya utunzaji wa mazingira haitatekelezeka.

Mbali na hilo amesema  anasikitishwa na tabia ya viongozi wa serikali kujichukulia sheria mikononi kwa kufyeka mazao ya wakulima.

Aidha,kauli hiyo  ilitokana na mwenyekiti huyo kuwatetea wananchi ambao wanaishi katika mlima kiboriani ambako kunadaiwa kuna vyanzo vya maji.

Nyaulingo ambae pia ni Diwani wa (CCM) Kata ya Rudi amesema  kumezuka mtindo wa viongozi wa serikali kukurupuka na kuingia katika mashamba ya wakulima na kuanza kufyeka mazao yao kwa madai kuwa wamelima katika maeneo ambayo hayakubaliki.

“Hebu jiulize mkulima anapoanza kulima anafuata hatua mbalimbali, anafyeka misitu, anachoma takataka anaanza kulima anapanda mbegu na kupalilia hadi mazao yanakomaa.

“Cha kushangaza mazao yakisha komaa wanajitokeza watumishi wa serikali na kudai kuwa mtu huyo amelima katika maeneo ambayo hayaruhusiwi jambo la kujiuliza watumishi hao walikuwa wapi kama si kutaka kutengeneza hisia za kuwepo kwa dalili za kutaka kupokea rushwa” amesema Nyaulingo .

Amesema  uharibifu wa mazingira unaenda sambamba na umasikini hivyo ili kuondokana na uharibifu huo ni lazima wananchi wakatafutiwa njia mbadala ya kuwaondoa katika umasikini.

error: Content is protected !!