June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Serikali ijipange kudhibiti dawa za kulevya’

Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (Kulia) akizungumzia kuhusu umuhimu wa serikali kutumia Sheria Mpya ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya wakati wa mahafali ya mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) leo. Kushoto ni Jama Gulaid Mwakilishi Mkazi wa UN na Mkuu wa UNCEF – Shirika la Watoto Duniani nchini Tanzania.

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kujipanga ili kudhibiti biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya. Anaandika Pendo Omary… (endelea).

Hatua hiyo ni utekelezaji wa Sheria mpya ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za Kulevya ya mwaka 2015 (The Drugs Control and Enforcement Act, 2015), baada ya kupitishwa na Bunge hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na George Masaju – Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa mahafali ya mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).

Masaju amesema, “Tangu mwaka 1980 tatizo la dawa za kulevya limekuwa kwa kasi nchini. Mwaka 1985, Bunge lilitunga sheria na kuanzisha Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya”

Amesema “licha ya kuwepo tume hiyo, zilijitokeza changamoto za kimfumo. Serikali imeona umuhimu wa kuwa na sheria mpya. Hivyo ni lazima kujipanga ili kutekeleza sheria hii”

“Sheria iliyopo haijaharamisha baadhi ya vitendo vinavyohusiana na biashara ya dawa za kulevya, vikiwemo kumiliki mitambo au maabara kwa lengo la kutengeneza dawa za kulevya. Sheria mpya imeharamisha umiliki huo na kuweka adhabu kali ya kifungo cha maisha na faini siyopungua Sh. 200 milioni,” amesema Masaju.

Aidha, Jama Gulaid- Mwakilishi Mkazi wa UN na Mkuu wa UNCEF – Shirika la Watoto Duniani nchini Tanzania, amesema taarifa ya Jeshi la Polisi inaonesha kati ya mwaka 2010 na 2013, Jeshi hilo lilikamata kilo 742 za heroin, kilo 348 za cocaine, kilo 77 za bangi na kilo 16 za mirungi.  

Gulaid amesema “Pia kuna ripoti zinaonesha watanzania kukamatawa na kuwekwa kizuizini kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika nchini nyingi duniani zikiwemo Mauritius, Falme za Kiarabu, China, Brazil na Afrika Kusini.”

“Hivyo, program hii ilikuwa na malengo ya; kuwajengea uwezo waandishi wa habari waandamizi na wahariri kuwa na uelewa wa kina kuhusu matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya na kuwawezesha kuandika mara kwa mara kuhusu madawa ya kulevya.” Amesema Gulaid.

Gulaid ametaja lengo lingine kuwa ni kuhamasisha mabadiliko chanya katika jamii hasa vijana.

Aidha, Deodatus Balile – Mwandishi wa Gazeti la Jamhuri ambaye pia amenufaika na mafunzo hayo amesema “Baada ya waandishi 9 kutoka katika mradi huu kufanya uchunguzi wa kihabari kuhusu biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya imesaidia serikali kupitia Bunge kutunga sheria mpya ya kudhibiti biashara hii.”

Mafunzo hayo yaliyoanza June na kumalizika Novemba 2014, yalifadhiliwa na UN, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania na kushirikisha waandishi wa habari 19.

 

error: Content is protected !!