July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali: Hatujafukuza wafanyabiashara wa kigeni

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imekanusha kuwafukuza raia wa kigeni waliokuwa wakifanya biashara zao nchini na kuwa haina mpango wakufanya hivyo. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya amesema kuwa tamko hilo linatokana na taarifa zisizo za kweli zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli amewafukuza wageni hao kwa kuwa serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.

Irovya, bila ya kuwataja waliohusika na kutuma taarifa hizo mitandaoni, amesema taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kufuatia idara ya Uhamiaji kuanza kutekeleza jukumu la kufuatilia wageni wanaoishi nchini bila vibali halali vya ukaazi kwa mwezi Novemba na Desemba mwaka jana.

Amesema taarifa zinazoenezwa ni za kuzusha, hazina ukweli wowote na nia njema kwa nchi kwani kati ya 2014 na 2016 Idara ya Uhamiaji imetoa vibali vya ukaazi (Residence Permits) 40,765 kwa wageni wawekezaji na wafanyabiashara wageni.

“Wageni 372 waliondoshwa nchini katika miezi hiyo miwili kwa kutokuwa na vibali halali vya ukaazi hata hivyo Idara ya Uhamiaji tangu Januari hadi Desemba mwaka jana, iliondosha wageni 1,642 waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli zao nchini kinyume na sheria.

“Pamoja na hilo Serikali inakaribisha wageni kuja nchi kuwekeza na kufanya shuguli zao kwa kufuata sheria,” amesema Irovya.

 

error: Content is protected !!