May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali hatarini kupoteza 100 Bil, Mdee amkaba Lukuvi

Halima Mdee, Mbunge wa Chadema Viti Maalim

Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalum asiye na chama bungeni, Halima Mdee, amesema Serikali iko hatarini kupoteza Sh. 100 bilioni, endapo itavunja mkataba wa mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wa ujenzi wa nyumba (711 na 712), katika Jimbo la Kawe, mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Jemima Samweli, DMC … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Jumatano tarehe 26 Mei 2021, Mdee amesema kuna hati hati ya fedha hizo kupotea, kwa kuwa hadi sasa hakuna dalili za NHC kutekeleza mradi huo, kufuatia hatua ya Serikali kuinyima kibali cha kukopa fedha za kuuendesha.

Katika mjadala huo wa Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mwaka 2021/22, Mdee amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ampe majibu juu ya suala hilo.

“Tusipotekeleza mkataba mnaenda kulipa Sh. 100 bilioni, wakati mmekataa kuipa ruhusa NHC kukopa fedha, yaani Sh. 100 bilioni unaenda kumpa mkandarasi kwa kuvunja mkataba? Nakuomba unipe majibu yenye mantiki, kwa maslahi mapana ya nchi na Jimbo la Kawe,” amesema Mdee.

Mdee alimtaka Lukuvi kumpa majibu hayo, baada ya kubaini waziri huyo hajatekeleza ahadi yake, iliyosema wizara yake itaweka fedha katika bajeti ya mwaka 2021/2022, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
“Juzi niliuliza swali, waziri akajibu akasema mradi huu utakuwepo kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha, na kwamba tuna anza kutekeleza. Sasa kama mwaka wa fedha huu, lazima kwenye maandishi huku nione lakini sijaona,” amesema Mdee.

Wiliam Lukuvi, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Jamii

Mdee amesema, 2014 NHC iliingia mikataba wa utekelezaji miradi hiyo wenye thamani wa Sh. 245 bilioni (Sh. 142 bilioni kwa mradi 711 na Sh. 103 bilioni kwa mradi 712), ambapo mmoja umetekelezwa kwa asilimia 20 na mwingine 30, kisha kukwama baada ya shirika hilo kukosa fedha.

“Mradi mmoja umetekelezwa kwa asilimia 20, mwingine asilimia 30. Mkataba wa kwanza ulikuwa 2014 hadi 2017, mkaongeza muda mpaka 2019, leo kazi imelala. Lakini CAG anasema ule mkataba ulikwama kwa namna shirika linavyojiendesha kibiashra.

Kwamba Limegota, limeshindwa kupewa hela sababu wamekopa na mwisho wa ukomo wao kukopa ni Sh. 300 nilioni, wakaenda kuomba kibali Wizara ya Fedha toka 2017, kwa sababu mradi huu una faida, mpaka leo hawajapewa,” amesema Mdee.

Mdee amesema kukwama kwa mradi huo, kumesabisha hasara kwa baadhi ya wananchi waliolipa fedha, kwa ajili ya kununua nyumba hizo baada ya kujengwa.

“Nini kimetokea, kuna wananchi wamewekeza Sh. 3 bilioni, wale wameshanunua wametoa fedha kabla hazijajengwa. Waziri unatuambia tuna pesa ni kweli?” Amesema Mdee.

Mdee ameishauri Serikali iutekeleze mradi huo, kwani una manufaa hususan kipindi hiki kuna uhaba wa nyumba za kupanga.

“Tafiti zinaosnhea tuna upungufu wa nyumba kwenye majiji wa zaidi ya milioni tatu, na kila mwaka nyumba laki mbili zinahitajika. Halafu mnakaa hapa mnasema hatuna mapato,” amesema Mdee na kuongeza:

“Yaani hatuna mapato wakati pale Kawe New City, iiliyokuwa inatarajiwa kuwa na wakazi 50,000 ingekuingizia mapato. Kwa nini tunafikria kiumsikini?”

error: Content is protected !!