July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali haiwezi kupambana na rushwa kwa msaada

Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea

Spread the love

SERIKALI imesema haiwezi kuomba msaada wa kupambana na rushwa kutoka nchi nyingine kwa kuwa Tanzania Taifa huru na lililojitosheleza. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa bungeni leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (Chadema).

Katika swali lake Nyerere aliitaka Serikali kuomba msaada wa kumbana na rushwa kutoka nchi zilizofaulu kwa kuwa inaonyesha jitihada za nchini za kupambana na tatizo hilo zimeshindwa.

Mkuchika amesema sio kweli kwamba Serikali imeshindwa kupambana na rushwa na kwamba jitihada zimekuwa zikifanyika na zimezaa matunda.

“Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) , ilifanikiwa kuokoa Sh. bilioni 12.6, Tanzania ni Taifa huru halihitaji mtu yoyote kuja kutusaidia kupambana na rushwa,” alisema Mkuchika.

Akijibu swali la Mbunge wa Wawi,(CUF) Hamad Rashid Mohamed , Mkuchika alisema Serikali imeiiagiza Wizara ya Fedha kuleta mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi.

Amesema katika mapendekezo hayo nadhani suala la kufanya manunuzi ya Serikali kupitia Teknolojia ya Habari (TEHAMA) litazingatia.

Hamad aliitaka Serikaliu kueleza lini itaanza kufanya manunuzi kwa TEHEMA ili kupunguza mianya ya rushwa katika manunuzi.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau (CUF), Mkuchika alisema Serikali inayo mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya vitendo vya rushwa.

“Kuongeza wigo wa wadau wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kushirikisha wizara, idara, wakala wa Serikali, serikali za mitaa, asasi za kiraia, mashirika ya dini, vyama vya siasa vyombo vya habari na sekta binafsi,”Amesema

Katika swali lake Mwidau alitaka kujua mikakati ya Serikali ya kulinusuru Taifa na janga la rushwa.

error: Content is protected !!