January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali haina uwezo wa kutoa ruzuku kwa wakulima

Mkulima mdogo mdogo wa Hanang

Spread the love

SERIKALI imesema haina uwezo wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wote nchini wakiwemo wa Jimbo la Busanda. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati akijibu swali la Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba (CCM).

Katika swali lake Bukwimba alitaka kujua mpango wa Serikali wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa Jimbo lake.

Zambi amesema utaratibu wa kutoa ruzuku umezingatia ukweli kuwa mpango huo suo endelevu.

“Serikali haina uwezo wa kibajeti wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wote nchini wakiwemo wa Jimbo la Busanda,” amesema.

Amesema kuwa serikali inatambua juhudi za wakulima wa jimbo hilo na Mkoa wa Geita katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo nchini.

“Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa Mkoa wa Geita na Jimbo la Busanda ambapo kati ya mwaka 2010/11 na 2013/14 jumla ya vocha 300,888 zenye thamani ya Sh. bilioni.76 zimenufaisha kaya 100,296,” amesema.

Amesema vocha hizo ni za ruzuku ya mbegu za mahindi, mpunga na mbolea ya kupandia na kukuzia.

Amesema utaratibu wa utoaji ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa wakulima umeweka vigezo mbalimbali kwa wanufaika ikiwemo uwezo wa kuchangia gharama za pembejeo husika kwa lengo la kuwajengea wakulima uwezo na mazoea ya kujinunulia pembejeo wenyewe.

error: Content is protected !!