Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali haimjui aliyebuni Nembo ya Taifa
Habari za SiasaTangulizi

Serikali haimjui aliyebuni Nembo ya Taifa

Spread the love

SERIKALI imesema mpaka sasa haijafahamika ni nani aliyebuni nembo ya taifa tofauti na ilivyokuwa ikijulikana kuwa aliyebuni nembo hiyo ni Francis Ngosha (80) yaliyekufa hivi karibuni, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Devotha Minja (Chadema).

Akiuliza swali la nyongeza bungeni Minja amesema inawezekanaje serikali inajidai kuwa inalinda haki za wasanii wakati serikali hiyo hiyo imemdhurumu marehemu Francis Ngosha ambaye alibuni nembo ya taifa na kumsababishia kufa akiwa masikini.

Katika swali la nyongeza pia amesema inakuwaje serikali iliyopo madarakani imekuwa ikishangilia na kuchekelea pale wasanii wanapotunga nyimbo za kuvikejeri vyama vya upinzani lakini pale ambapo wanasanii wanapoimba nyimbo za kuikosoa serikali wasani hao wamekuwa wakishugulikiwa mfano akiwa Ney Wamitego na Roma Mkatoliki.

Awali katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua mpaka sasa ni hatua gani zimechukuliwa kwa watu ambao wanahujumu kazi za wasanii.

“Mchango wa kazi za wasanii unaonekana kutoa ajira lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kuhujumiwa kazi zao.

“Mheshimiwa rais ametoa maagizo mbalimbali ya kushughulikia watu wanaohujumu kazi za wasanii, Je mpaka sasa ni hatua gani zimechukuliwa?” alihoji Minja.

Akijibu maswali hayo Wambura amesema kuwa mpaka sasa haijajulikana ni nani ambaye alibuni Nembo ya taifa kwani mpaka sasa wapo watu watatu ambao wanasadikiwa kuwa walibuni nembo ya taifa.

Amesema kuwa inaonesha kuwa marehemu Ngosha yeye hakuwa mbunifu bali alikuwa anakipaji cha uchongani na uchoraji na wala siyo ubunifu.

“Wapo wanaosema kuwa aliyebuni nembo ya Taifa alikuwa ni Abdallah Fahani ambaye alibuni nembo ya Tanzania Kenya na UN, hivyo inasemekana kuwa marehemu ngosha alikuwa na uwezo wa uchoraji na uchongaji lakini siyo ubunifu.

“Wizara imeagiza kuhakikisha wataalamu wanafanya utafiti kuhakikisha wanafuatilia kuona ni nani rasmi ambaye aliweza kubuni nembo ya taifa na kwa maana hiyo serikali haijamdhurumu marehemu Ngosha kama inavyoelezwa,” amesema Wambura.

Katika hatua nyingine Wambura amesema ili kuhakikisha wasanii wanapata haki zao ni vyema wakajiorodhesha ili wasiweze kuhujumiwa kazi zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za SiasaTangulizi

Mkataba wa Tanesco, Songas watakiwa bungeni

Spread the loveWAKATI mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya Shirika la...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

error: Content is protected !!