July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali, Benki ya Dunia kujenga miundombinu Temeke

Spread the love

SERIKALI kwa kushirikiana na Benki ya Dunia katika siku za karibuni imepanga kuanza ukarabati wa miundombinu mibovu hususan mitaro kwa kuwa inachangia kusababisha maafa wilayani Temeke, Dar es Salaam, anaandika Aisha Amran.

Hayo yamesemwa leo na Joyce Msumba, Ofisa Habari wa Wilaya Temeke alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota, Shule ya Sekondari Kibasila na Mtaa wa Butiama ambapo inaelezwa chanzo chake kuwa ni ubovu wa miundombinu hiyo.

“Ni kweli maafa hayo yametokea   na sababu kubwa ni miundombinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika maeneo ya makazi ya watu, kwa hiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi yanapo stahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu, “ amesema Msumba.

Amesema ukarabati huo wa mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es Salam Metropolitian Development Projecct (DMDP) na unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Aidha Msumba amesema, endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza , watatumia njia za kunyonya maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea.

Mradi huu unalenga kuhamisha njia za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende huko.

error: Content is protected !!