July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali awamu ya tano itekeleze haya – Wanawake

Spread the love

KWA kuwa wanawake wanapenda uhuru na hawapendi kukandamizwa, ni lazima wapigane bila kupumzika mpaka madai yao yatakapotekelezwa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Hapa ndipo mkazo unawekwa na wanawake walio kwenye mapambano haya kwamba, agenda ya uwezeshwaji wa wanawake iwe kipaumbele kitakachozingatiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uchaguzi iliyozinduliwa tarehe 1 Septemba mwaka huu chini ya uratibu wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi Tanzania na TGNP Mtandao, wanawake wanaitaka Serikali ya Awamu ya Tano izinagtie mambo yafuatayo;

Katiba itakayobeba misingi ya haki za wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni ili waweze kupata haki sawa za uraia, siasa na uchumi na ustawi wa jamii, zitakazolindwa kikatiba.

Iweke mikakati endelevu itakayobatilisha sheria zote za ubaguzi wa jinsia ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mpya zitakazolinda utu wa mwanamke na kukataza mwendelezo wa tabia, taratibu na mila zenye kubagua na kuwakandamiza wanawake na watoto wa kike.

Aidha, serikali ijenge mkakati maalum utakaoondoa ukatili wa kijinsia ndani ya ndoa, ukeketaji, ndoa za utotoni, rushwa ya ngono, ubakaji na vitendo vingine vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike.

Iwe na mikakati endelevu na inayotekelezeka. Itakayojenga misingi ya usawa wa kijinsia katika ngazi zote za uongozi na maamuzi.

Serikali ichukue hatua madhubuti za kisera na kisheria ili kuhakikisha wanawake wanashiriki kwa uwiano sawa katika nyanja zote za uongozi pamoja na mihimili mikuu mitatu ya uongozi (Serikali, Bunge, na Mahakama) kwa kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa.

Ijenge mikakati itakayomhakikishia mwanamke haki ya uzazi salama nchini. Iwekeze zaidi katika afya ya uzazi kwa ujumla kwa kutambua mzigo mkubwa anaobebeshwa mwanamke kwa kuendeleza kizazi cha Tanzania na kuashiria kuweka rehani haki yake ya msingi ya kuishi

kutokana na changamoto anazokumbana nazo wakati wa kutimiza jukumu la uzazi.

Iweke mikakati na taratibu za kuwezesha wanawake kufikia, kutumia, kunufaika na kumiliki rasilimali za umma pamoja na ardhi, madini na miundombinu.

Itambue na kutekeleza haki za wanawake wenye ulemavu kwa kutambua kwamba huathirika maradufu na mfumo dume na mifumo yote kandamizi. Pia ichukue hatua za kisera na kisheria kulinda wanawake wenye ulemavu dhidi ya vitendo vya ukatili;

Kuhakikisha wanafikia huduma za msingi za kukimu maisha kama vile huduma za afya, elimu, hifadhi ya jamii na kutokubaguliwa katika ajira.

Iweke mikakati endelevu ya kuhakikisha haki sawa kwa wanawake za kufikia huduma za msingi ikiwa ni pamoja na maji, afya, elimu, huduma za hifadhi ya jamii kwa kutambua mahitaji maalum ya watoto wa kike, watu wenye ulemavu, wazee na makundi mengine katika jamii.

Ili madai yaliyotajwa hapo juu yatekelezeke, serikali iweke mikakati na taratibu thabiti na endelevu zitakazowezesha kila sekta kutenga bajeti zake kwa mtazamo wa Kijinsia (Gender Badget). Hii

iandamane na kujenga uwezo wake wa kufikisha azma hii katika utekelezaji wenye manufaa.

Iweke utaratibu endelevu wa kutekeleza mikataba yote iliyoridhia kuhusu haki za wanawake, mikataba hii itambulike kwamba ni sheria za nchi ili kuepusha ucheleweshwaji wa kutafsiri au kuruhusu tafsri zinazokinzana na misingi ya mikataba husika.

Ihakikishe kuwepo kwa sheria ya uuandaji wa mahakama za familia ili kufanikisha upatikanaji wa haki kwa wanawake kwa wakati unaofaa.

Madai kwa vyama vya siasa

Kwenye andiko hilo, vyama vinavyoomba ridhaa ya uongozi kutoka kwa wananchi vikitekeleza madai yafuatayo:-

Ilani au ajenda kuu za vyama zitambue na kudhihirisha kinagaubaga masuala muhimu ya kimaendeleo ya wanawake yatakayowapelekea kufikia na kunufaika na sera za nchi kama kufikia huduma za msingi, na pia kuwezesha kushughulikiwa kwa vikwazo mbalimbali vya kijinsia vinavyopelekea kumnyima mwanamke fursa na haki zao kama vile Ukatili wa Kijinsia.

Vijenge na kutekeleza mikakati thabiti na endelevu ya kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu na kulinda haki zao katika mchakato mzima wa uchaguzi zikiwemo uteuzi, kampeni, kupiga kura na baadaye.

Iwe marufuku kwa chama chochote kumbagua mwanachama kwa misingi ya jinsi, maumbile, dini, ukabila, kanda, hali au fikra mbadala.

Kuzingatia kanuni za maadili ya uchaguzi ili kujenga heshima na utu wa wagombea, hasa wanawake, wakati wote na kuonesha nia ya kujenga na kuimarisha amani

na umoja wa kitaifa.

Vyama vya siasa vioneshe nia ya kweli ya kupambana na ufisadi na rushwa za aina zozote zile ikiwa ni pamoja na rushwa ya ngono.

error: Content is protected !!