Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sera za Lissu Ulaya hizi hapa
Habari za SiasaTangulizi

Sera za Lissu Ulaya hizi hapa

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki yupo ziarani Ulaya na sasa ameanza kueleza sera zake pale atakapochaguliwa na Watanzania kuwa rais wao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Lissu akitokea Ubelgiji baada ya kupata matibabu yaliyotokana na majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa Dodoma, Tanzania Septemba 7, 2017 ameeleza namna taifa hili linavyopaswa kuwa katika utawala wake.

Akizungumza na Kituo cha Kimataifa ya Habari nchini Uingereza-BBC Swahili (Dira ya Dunia) Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema, taifa linapasa kuundwa kwa mfumo ambao yoyote atakayeingia madarakani ataweza kudhibitiwa.

Amesema kuwa, haya yote yanaweza kufanywa kwa kuundwa kwa Katiba imara inayoweza kumwongoza hata shetani ambaye naye akipinda, ataweza kudhibitiwa.

Sera ambayo ambayo Lissu ametilia mpakazo ili kuleta usawa kwenye taifa ni utawala ambayo unaheshimu haki za binadamu, uhuru wa watu, ubinadamu pamoja na heshimu mamlaka ya wananchi.

Alipouliza utofauti wake na uongozi uliopo sasa Lissu alisema, “… ni kujenga nchi yenye misingi ya kikatiba, ya kiutawala ambayo inaheshimu haki za binadamu, uhuru wa watu, ubinadamu, inaheshimu mamlaka ya wananchi.

“Ni muhimu zaidi kuwa na nchi yenye mifumo imara ya kikatiba ambayo ukimpata Trump (Donald Trump, Rais wa Marekani) atadhibitiwa, ukimpata shetani atadhibitiwa, ukimpata malaika vile vile atafanya mema yake lakini akigeuka atadhibitiwa.”

Kwenye mahojiano hayo na BBC Lissu amesema, tatizo kubwa na la miaka yote ni mfumo wetu (Tanzania) wa kisiasa na kikatiba ambao unaweza kuitwa ‘urais wa kifalme.’

“Hatuhitaji ufalme katika Karne ya 21, tunahitaji nchi rais akiwa mbaya inakwenda, akiwa mzuri atakwenda,” amesema Lissu.

Kiongozi huyo wa Singida na mwanasheria mahiri nchini amesema kuwa, namna ya kufikia malengo yake inategemea na ridhaa ya chama chake kwa kuwa, kina mfumo wa kumsimamisha mgombea.

Na kwamba, ikiwa chama chake-Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- kitaona anaweza kuwania nafasi hiyo, atakuwa radhi na kwamba, kama kitaona bado kwa sasa nalo atakubaliana nalo.

“Inawezekana kabisa kwamba kwenye vikao vya chama, wanachama na viongozi wenzangu wakasema kwamba, bwana Lissu pengine labda hutoshi, nitakubali uamuzi wao.

“Inawezekana wakasema Mzee Lowassa (Edward Lowassa) hebu muachie huyu kijana apambane katika haya mapambano ya sasa makali kidogo yanahitaji nguvu zaidi, hebu msaidie huyu kijana kwenye hili jukumu. Chochote kinawezekana, ni maamuzi ya vikao halali vya chama,” amesema Lissu.

Pamoja na malengo yake, Lissu ameeleza kuwa miongoni mwa mambo mema yaliyofanywa na utawala wa sasa ni pamoja na kufundisha thamani ya binadamu.

“…amefanya mazuri mengi, moja wapo ametufundisha thamani ya haki za binadamu kuliko rais mwengine yoyote tangu mwaka 61 tulivyopata Uhuru, ametufundisha thamani ya haki za binadamu ametufundisha thamani ya uhuru,” amesema Lissu.

Baada ya kuzungumza Uingereza, baadaye Lissu anatarajiwa kuendelea na ziara kwenye Ofisi za Umoja wa Ulaya (EU) zilizopo Brussels, Ubelgiji na baada ya hapo atakwenda Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!