November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Sera ya elimu bure haijaeleweka’ 

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

IMEELEZWA kuwa, wazazi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu sera ya elimu bure jambo ambalo linasababisha wanafunzi kushindwa kuendelea vyema na masomo. Anaripoti Danson Kaijage, Handeni … (endelea).

 Hayo yamebainishwa baadhi ya viongozi wa kata ya vibaoni, wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wipokuwa wakizungumza na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met) wakati wa Wiki ya Elimu iliyofanyika kitaifa wilayani humo.

 Ofisa Elimu, Kata ya Vibaoni wilayani humo Flora Marambo amesema, sera ya elimu bure imesababisha wazazi wengi kujiweka kando na watoto wao kwa kisingizio kuwa, wanatakiwa kuhudumiwa bure na serikali kwa kila kitu.

 Amesema, kutokana na uelewa mdogo kwa baadhi ya wazazi juu ya sera ya elimu bure, imefika hatua ya wazazi kutokuwa tayari kuwanunulia wanafunzi mahitaji muhimu kwa madai kuwa, serikali itafanya.

 “Tatizo la uelewa kwa baadhi ya wazazi juu ya sera ya elimu bure ni tatizo kubwa kwa Wilaya ya Handeni hususani katika Kata ya Vibaoni, wapo wazazi ambao wanafikia hatua ya kutokuwa tayari kuwanunulia wanafunzi wao madaftari kwa madai kuwa, kwa sasa elimu bure.

 “Kutokana na baadhi ya wazazi kutioielewa vizuri sara ya elimu bure, imesababisha baadhi ya wanafunzi kutofanya vizuri au kutofika mashuleni kutokana na kutokuwa na vifaa muhimu vinavyotakiwa shuleni.

 “Wapo wazazi ambao wanakataa kuwanunulia watoto wao, vifaa vya shule kwa maelezo kuwa kuwa serikali imeisha tangaza kwamba watoto wote wanatakiwa kupata elimu bure,” amesema.

 kutokana na hali hiyo serikali kwa kushirikiana na wadau wa Elimu wameombwa kutoa elimu kwa wazazi na kutoa tafsiri sahihi juu Sara ya Elimu bure ili kuondoa mgongano uliopo kwa sasa.

 Maadhimisho ya Wiki ya Elimu yanaendelea Wilayani Handeni Mkoani Tanga huku,huku Mtandao wa Elimu Tanzania wakifanya ziara ya mashuleni wakiibua changamoto za elimu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

error: Content is protected !!