August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Senzo atimka Yanga, Simon Patric achukua mikoba yake

Spread the love

 

KAMATI tendaji ya klabu ya Yanga imebadiliki ombi la kutoongeza mkataba ambalo liliwasilishwa na mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Senzo Mbatha. Anaripoti kelvin Mwaipungu…(Endelea)

Kikao hiko cha kamati tendaji kilifanyika hii leo kwa mara ya kwanza, kikongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa muda mfupi na klabu hiyo, ilieleza kuwa Afisa huyo raia wa Afrika Kusini amekacha kuongeza mkabata wake ambao unamalizika tarehe 31 Julai 202, kutokana na sababu za kifamilia.

Mara baada ya kuridhia ombi hilo kamati hiyo iliamua kumteuwa Wakili wa klabu hiyo Simon Patrick kuwa mtendaji mkuu wa muda.

Senzo alijiunga na Yanga mwaka 2019 mara baada ya kujiuzuru nafasi yake ya utendaji mkuu ndani ya klabu ya Simba mabyo ilimleta nchini kwa mara ya kwanza.

error: Content is protected !!