HALI ya wasiwasi nchini Senegal, imezidi kutanda baada ya Ousmane Sonko (46), kiongozi wa upinzani kutuhumiwa kubaka. Mtandao wa Aljazeera unaripoti … (endelea).
Serikali ya nchi hiyo, ilimkamata Sonko Jumatano wiki iliyopita, bila kueleza sababu jambo lililosababisha kuibuka kwa maandamano.
Hata hivyo, kiongozi huyo alifikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii ambapo pamoja na makosa mengine, ameyotuhumiwa kubaka.
Wafuasi wa kiongozi huyo wengi wao wakiwa vijana, wameghadhibika na hatua ya Sonko kutuhumiwa ubakaji ambapo wameeleza “ni hila za serikali (ya nchi hiyo) ili kumzima.”
Maandamano makubwa yametikisa mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar Jumatatu na kuendelea mpaka sasa. Maduka na huduma zingine zimefungwa ‘kupisha’ rapsha hiyo.
Polisi wa Senegal wamekuwa wakitumia nguvu ikiwemo maji ya washa na mabomu ya machozi kukabili maelfu ya waandamanaji hao.
“Hatuwezi kuruhusu Macky Sall (rais) akakandamiza demokrasia na kumfunga mpinzani wake,” Rama Diop (30), amenukuliwa na Aljazeera akiongeza “Ousmane Sonko anawakilisha matumaini ya maisha bora Senegal.”
Watu watano wanaripotiwa kupoteza maisha kwenye maandamano hayo, tangu yalipoanza Jumatano wiki iliyopita.
Leave a comment