May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Selikali yaanza kutekeleza yaliyoachwa Hayati Magufuli

David Silinde, Naibu Waziri TAMISEMI

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, imeanza kutekeleza ahadi zote zilizoachwa na mtangulizi wake, Hayati John Pombe Magufuli. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde, leo Jumanne tarehe 27 April 2021, bungeni jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu.

Silinde alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Buyungu (CCM,) mkoani Kigoma, Aloyce Kamamba, aliyehoji serikali ni lini itakuwa tayari kutekeleza ahadi zilizoachwa na Hayati Magufuli.

“Mwaka 2015 wakati wa kampeni, Rais (Hayati Magufuli), alihaidi kujenga barabara ya kilomita tatu mji wa Kakonko ambao ndiyo makao makuu ya wilaya je, kwanini ahadi hiyo haijatekelezwa na ni lini sasa itatekelezwa,” aliuliza Kamamba.

Akijibu swali hilo, Silinde alisema, serikali imeanza kutekeleza ahadi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Magufuli kwa awamu katika mwaka wa fedha 2020.

“Serikali imeanza ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 630 kwa kiwango cha lami katika mji wa Kakonko itakayogharimu Sh.500 milioni,” alisema Silinde.

“Mpaka sasa, ujenzi huo umefikia asilimia 80 na mradi unategemea kukamilika Mei 2021,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema, serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara nchini ikiwemo wilaya ya Kakonko kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

Katika swali la nyongeza, Kamamba ameuliza “ujenzi huo ni wa muda mrefu, miaka sita imepita mpaka sasa, lakini vile serikali imeweza kutoa majibu utekelezaji wake wameweka kifusi katika mji huo wa Kakonko.

“Ni miezi minne sasa shughuli za kibiashara katika mji huo hazifanyiki Je, Serikali ipo tayari angalau kifusi kiweze kusawazishwa katika maeneo hayo ili wananchi wakaendelea na shughuli zao za kijamii wakati taratibu nyingine zikifanyika?

Silinde alijibu swali hilo akisema, barabara hiyo inajegwa kwa kiwango cha lami na kifusi ambacho kimewekwa ni moja wapo ya njia ya kukamilisha ujenzi huo, kwa hiyo mpaka kufikia Mei 2021, ujenzi huo utakuwa umeshakamilika kwa sababu Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) wapo kazini.

error: Content is protected !!