Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Selikali: Tunatoa elimu inayotatua matatizo ya Mtanzania
Elimu

Selikali: Tunatoa elimu inayotatua matatizo ya Mtanzania

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Josephat Kandege
Spread the love

SERIKALI imesema kuwa elimu inayostahili kutolewa nchini ni ile ambayo inajikita katika kutatua matatizo yote na ambayo ni bora na siyo bora elimu. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Josephat Kandege, wakati wa Ufunguzi wa kongamano la Elimu la kila Mwaka lililofanyika Jijini Dodoma.

Kongamano hilo lilijumuisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, wazazi, Chama cha walimu, Maofisa wa Tamisemi, Maofisa wa Wizara ya elimu, Wakurugenzi wa halmashauri, Necta, Veta na Nacte.

Kandege alisema kuwa alisema kuwa ili kuwa na elimu bora ambayo inaweza kutatua matatizo mbalimbali ni lazima wadau wa elimu pamoja na elimu wakionyesha biidii katika utendaji kazi wao kwa manufaa ya taifa na Kizazi kijacho.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet) kwa kushirikiana na Right to Play  ambapo kauli mbinu yake ni “Ulinzi wa Mtoto ni wetu sisi wote” Kandege alisema kuwa elimu ya Tanzania inatakiwa kuboreshwa na kuwa elimu bora katika Afrika Mashariki.

Kandege alisema kuwa Serikali imeamua kuwekeza katika suala la elimu kwa Shule za serikali ili kuhakikisha kiwango cha elimu kina kuwa bora zaidi tofauti na ilivyo kuwa hapo awali.

Katika hatua nyingine Kandege alisema kuwa wanafunzi wafundishwe uhalisia wa maisha ili kufamfanya mwanafunzi aweze kuwa na ujasiri wa kujiamini na kujifunza kwa njia ya ushindani wa kuelimika kwa nchi za jirani.

Alisema iwapo elimu itaboreshwa kwa watoto wa kitanzania itasaidia watoto hao kuwa safi, kuakiri, kiuchumi na kimaadili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za SiasaTangulizi

Walimu 12,000 kuajiriwa mwaka huu, wa kike kupewa kipaumbele

Spread the loveKATIKA mwaka 2023/2024, Serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 wa masomo...

ElimuHabari za Siasa

Ukomo michango wanafunzi kidato cha tano 80,000

Spread the loveSERIKALI imesema ukomo wa michango kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha...

ElimuHabari Mchanganyiko

Dk. Biteko apongeza mikakati ya kuinua elimu Dodoma

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko...

ElimuHabari za Siasa

Shigongo: Nafanya masters kwa kutumia kipaji pekee

Spread the loveMbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (CCM) ameishukuru Serikali kwa kurejesha...

error: Content is protected !!