January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sekta ya nyuki yaingiza dola milioni 2

Afisa Nyuki Mkuu Kitengo cha Masoko na Leseni, Mwanahamis Mapolu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

WAKALA wa Misitu Tanzania kitengo cha nyuki, umesema kuwa kila mwaka sekta ya ufugaji nyuki nchini huzalisha wastani wa dola za Kimarekani milioni 2 kutokana na mauzo ya asali na nta ndani ya nchi na nje ya nchi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Afisa nyuki mkuu, Mwanahamis Mapolu, amesema ukiachana na kuongeza kipato nchini pia ufugaji wa nyuki huongeza ajira kwa watu wengi.

Mapolu amesema kuwa, Tanzania inakadiriwa kuwa na hekta za misitu milioni 48 na mbuga zinazofaa kwa ufugaji nyuki na zaidi ya hekta 80,000 ni mashamba ya miti ambayo pia hufaa kwa ufugaji wa nyuki.

Kwamba, ufugaji nyuki unaweza kufanyika kwenye mashamba ya kilimo kama, maharage, alizeti, michungwa, mbogamboga na mazao mengine.

“Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya ufuga nyuki ya mwaka 1998 na sheria ya ufugaji Na 15 ya 2002 kwa pamoja, vinatoa fursa kwa watu mbalimbali kumiliki manzuki na hifadhi za nyuki nchini ili kuwawezesha wadau wengi zaidi kushiriki na kuhifadhi nyuki,” amesema.

Ameongeza kuwa, kwa mwananchi yoyote atakayetaka kufanya biashara ya nyuki ni lazima ajisajili, ambapo usajili utakuwa wa aina mbili wa mfanyabiashara wa ndani ya nchi na nje ya nchi.

Amefafanua kwamba, nyaraka muhimu za kupata usajili ni kuwa na leseni ya biashara toka wizara ya viwanda na biashara, cheti cha mlipa kodi, cheti kutoka TRA, picha mbili na usajili wa jina la biashara.

“Ada ya usajili na usafirishaji ili kufanya biashara ya nyuki ndani ya nchi ni Sh. 26,000, nje ya nchi Sh. 55,000 na ukaguzi wa bidhaa za kwenda nje kwa kiasi kisichozidi kilo 30, ukaguzi ni Sh. 5,000 na kibali Sh. 20,000,”amesema. 

Licha ya kitengo cha nyuki kuwa na faida nyingi nchini, lakini bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili wafugaji hao ikiwemo ya kukosa mitaji ya kufanya biashara na kukosa sapoti kutoka serikalini.

error: Content is protected !!